Na Mwandishi Wetu, Singida
TIMU ya soka ya mashabiki wa Li v e r p o o l n c h i n
i Uingereza wa mjini Singida, juzi imenyakua ubingwa wa bonanza la Serengeti
Fiesta mkoani hapa, baada ya kuichapa Bayern Munich ya Majengo mabao 2-0.Kwa ushindi huo, Liverpool
imejinyakulia kombe na sh. 300,000 taslimu. Mshindi wa pili Bayern Munich, wao
walizawadiwa sh. 200,000.
Mashabiki wa Liverpool wamewavua ubingwa huo wenzao wa Arsenal wa
mjini Kigoma, ambapo Arsenal walinyakua ubingwa huo kwa kuichapa Manchester
United.Mchezo huo mkali
na wa kusisimua, ulifanyika kwenye Uwanja wa Klabu ya Peoples uliopo Utemini
mjini Singida na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji huo na vitongoji vyake.
Mabao ya Liverpool
yalifungwa na Mohammad Said na Saidi Saidi katika dakika za 58 na 71.Bayern Munich itabidi wajilaumu wenyewe
kwa kukosa nafasi nyingi za kufunga kwani walikosa mabao ya wazi dakika za 61,
69 na 81 kutokana na safu yake ya ushambuliaji kutokuwa makini walipokuwa wakilikaribia
lango la wapinzani wao Liverpool.
Ak i z u n g umz a b a a d a y a
kumalizika mchezo huo, Meneja Biashara wa Kampuni ya bia ya Serengeti Kanda ya
Ziwa, Octavian Migire alisema wameamua kudhamini bonanza la Serengeti Fiesta
Soccer Bonanza kwani ni shamrashamra za awali, kabla ya tamasha kubwa la
Serengeti Fiesta mjini Singida kwa kuwa mchezo wa soka unajumuisha watu
mbalimbali ambao ni wateja wao.
Alisema kupitia michezo, vipaji
huibuka, kwani ni fursa kwao kuonekana na wadau wa soka ili wahusika waweze
kujiajiri na kuajiriwa."Kama unavyojua, ajira kupitia
michezo nafasi ni nyingi na hazina masharti magumu kama
zilivyo kwa kazi zingine. "Pia zinalipa mapato makubwa kuliko kazi zingine
zozote hapa duniani," alisema Migire
No comments:
Post a Comment