Na Grace Ndossa
DOLA za Marekani milioni 100
zinatarajiwa kutumika kununua mabasi ya Mradi wa Mabasi yaendayo kasi jijini
Dar es Salaam kwa upande wa sekta binafsi.Hayo
yalibainishwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Mifumo na Uendeshaji wa
DARTS, John Mashauri, wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana.
Alisema sekta
binafsi ndiyo itakuwa inahusika katika ukusanyaji wa nauli pamoja na utunzaji
wa fedha katika mradi huo ili kudhibiti upotevu wa fedha.Alisema zabuni
za ununuzi wa mabasi na uwekezaji kwenye mfumo wa ukusanyaji nauli na utunzaji
wa fedha zinafanyiwa mapitio zilingane na uhalisia kitakwimu na uendeshaji
kutokana na muda mwingi kupita tangu ziandaliwe.
"Utoaji wa
huduma kwenye mfumo wa wakala wa usafiri wa haraka unahusisha zaidi sekta
binafsi na unatarajiwa kuwekeza dola milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa mabasi
na mfumo wa ukusanyaji wa nauli na utunzaji wa fedha ambazo zinatakiwa kuwa
tayari mfumo unapoanza kufanya kazi," alisema Mashauri.
Alisema mradi
wa DARTS umepata mshauri Mwelekezi Mkuu ambaye atasaidia wakala kufanikisha
azma yake ya kukamilisha utekelezaji wa shughuli za ujenzi wa miundombinu na
upatikanaji wa watoa huduma katika mfumo huo.
Mashauri
alisema katika utekelezaji wa mradi huo awamu ya kwanza jumla ya daladala 1,600
zitahamishiwa sehemu nyingine kupisha mabasi yaendayo haraka katika jiji la Dar
es Salaam.Alisema kwa sasa
wanaandaa mkutano maalum wa wamiliki wote wa daladala ili kuendelea
kuwahamasisha wajiunge katika kampuni na baadaye wanunue hisa.
Akizungumzia kuhusu
fidia, alisema tayari wafanyabiashara 230 waliokuwa katika Kituo Kikuu cha
Mabasi Ubungo wamelipwa na wakazi wa Magomeni Bondeni 42 wamelipwa na kupisha
uhamisho wa nguzo za umeme.Kwa upande wa Kariakoo Gerezani,
alisema wakazi 81 kati 106 wamekwishalipwa fidia zao na baadhi yao bado
taratibu zinaendele
No comments:
Post a Comment