Na Frank Monyo
MAMLAKA ya Bandari Ta n z a n i a ( T
PA) , imeendelea kufanya maboresho katika utendaji kazi kwa upande wa Bandari
ya Dar es Salaam ili kuongeza ufanisi wakati wa kuwahudumia wateja wake.Akizungumza na gazeti hili ofisini
kwake jana, Meneja Mawasilino wa TPA, Janeth Ruzangi, alisema juhudu za pamoja
kati ya wadau na mamlaka zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi katika
bandari hiyo.
"Mafanikio yaliyopatikana ni
kuongezeka kwa shehena kutoka tani milioni 10.9 kwa mwaka 2011/12 hadi kufikia
tani 12.5 mwaka 2012/13 ikiwa ni ongezeka la asilimia 15.0 pia katika shehena
yote iliyohudumiwa mwaka 2012/13,shehena za chini zitumiazo bandari (landlocked
countries) ilikuwa tani milioni 4 ambayo ni sawa na asilimia 32 ya shehena,"
alisema Ruzangi.
Alisema shehena yote ya mizigo ya nchi
6 zitumiazo Bandari ya Dar es Salaam; za Zambia, Malawi, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Rwanda na Uganda imeongezeka kutoka tani
milioni 3.55 mwaka 2011/12 hadi kufikia tani milioni 4.05 mwaka 2012/13.
Alisema ongezeko hili ni asilimia 14.2.
Aliongeza kuwa muda wa ukaaji wa meli
bandarini umepungua kutoka siku 6 hadi siku 4 ambapo ni sawa na asilimia 19.7
wakati idadi ya siku kwa meli kusubiri nje kuingia ndani kwenye gati imepungua
kutoka siku 3 hadi kufikia siku 1 mwaka 2012/13 kinyume na siku 28
zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
"Hata hivyo, kasi ya kupakua
magari imeongezeka kutoka upakuaji wa magari 343 kwa shift hadi magari 672;
ongezeko hili ni asilimia 95.9," alisema Ruzangi.
Alibainisha
sababu za kuongezeka kwa ufanisi huo kuwa ni hatua zilizochukuliwa na serikali
kupitia Wizara ya Uchukuzi kwa kusimamia kwa karibu utendaji kazi wa mamlaka
hiyo.
No comments:
Post a Comment