JUMLA ya nchi saba za
ukanda wa mashariki mwa Afrika zinashiriki itikafu ya kimataifa iliyoanza juzi
visiwani Zanzibar.tikafu hiyo ambayo hufanyika kila
mwaka katika Msikiti wa Said wa Shoto uliopo Amaan mjini Unguja ilifunguliwa na
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Rashid Seif
. Ak i z u n g umz a k a t i k a ufunguzi
huo Seif alisema kuwa mkusanyiko huo ni ishara tosha inayoonesha umoja na
mshikamano wa waislamu kupitia mataifa mbalimbali.Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Itikafu
Zanzibar, Khatib Twahir alisema lengo la itikafu hiyo ni kuleta ushirikiano
baina ya waislamu bila ya kujali utaifa wake.
Nchi hizo zinazoshiriki katika itikafu
hiyo ni pamoja na Kenya, Uganda, Malawi,
Burundi, Rwanda na Zambia,
Tanzania bara na wenyeji wa Zanzibar.Hata hivyo, aliwataka Wazanzibari na
nchi jirani wakiwemo na wanafunzi kuhamasishana kushiriki katika ibada hiyo.
Sambamba na hivyo alisema kuwa bado
wanakabiliwa na upungufu wa fedha na kuwaomba waislamu wenye uwezo kuchangia
asilimia kumi iliyobakia ili kufanikisha itikafu hiyo.Hivyo aliwataka wananchi kuhudhuria kwa wingi katika itikafu hiyo ambapo
pamoja na mambo mengine madrasa mbalimbali zinashiriki katika mashindano ya
kuhifadhi Quran.
.
No comments:
Post a Comment