07 January 2013
Mexime ajivunia kushiriki Mapinduzi Cup
LICHA ya timu yake kutofanya vizuri kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendelea visiwani hapa, kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime amesema amepata kwa kuanzia kabla ya kuanza Ligi Kuu.
Kocha huyo alisema kupitia mashindano hayo ameijua vizuri timu yake na kugundua makosa mengi ambayo atayarekebisha ili kufanya vizuri kwenye michezo ya ligi kuu itakayoanza mwishoni mwa mwezi huu.
Mtibwa Sugar katika mashindano hayo imefungwa mechi moja 4-1 na Miembeni FC, ikato kasare ya 1-1 na Coastal Union katika mechi iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Amaan na kuifanya Mtibwa iwe na pointi moja huku kundi hilo B likiongozwa na Azam FC yenye pointi 4, Miembeni ina pointi 3 na Coastal ikiwa pointi 2.
Mexime alisema nafasi ya kusonga mbele ni finyu lakini amefurahi kupata nafasi ya kushiriki kwa kuwa amecheza mechi muhimu zilizomuonyesha makosa katika timu yake.
"Timu kufanya makosa inasaidia kujua kwa kuanzia kurekebisha kabla ya kuanza ligi kuu, wachezaji wangu hawakuwa makini kwa kuwa hatukujiandaa mapema lakini wamejitahidi" alisema Mexime.
Kocha huyo mzawa alisema baada ya kumaliza mashindano hayo wataanza maandalizi rasmi kwa ajili ya ligi kuu na kufukia makosa yote yaliyoonekana wakati huu ili kufanya vizuri kwenye michezo ya ligi kuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment