11 January 2013
Madiwani CCM wataka kuzipiga Polisi
Na Patrick Mabula, Chato
MADIWANI wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Halmashuari ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita, juzi walitaka kupigana mbele ya Kituo cha Polisi wilayani humo.
Mashuhuda wa tukio hilo, walisema madiwani hao walikwenda kituoni hapo kila mmoja akimlalamikia mwenzake kumtishia
maisha na kumdhuru kwa njia yoyote.
Mkuu wa Polisi wilayani humo, Bw. Leonard Nyaoga, aliwataja madiwani hao kuwa ni Bw. Ismail Luge (Kata ya Ilemela), na Bw. Barthoromeo Manunga (Kata ya Bongela).
“Madiwani hawa kila mmoja anamlalamikia mwenzake kumpa vitisho vya kutaka kumdhuru hata kutumia kemikali...kutokana na uzito wa suala lenyewe, tuliwataka waende katika chama chao ili wakayazungumze kabla ya kufunguliana mashtaka,” alisema.
“Bw. Luge alianza kufika kituoni na kufungua kesi akimtuhumu Bw. Manunga ambaye naye alikuwepo katika Ofisi ya OCD wakaanza kushambuliana kwa maneno na kutaka kupigana.
Inadaiwa kuwa, chanzo cha ugomvi huo ni baada ya Bw. Manunga kumwita Bw. Luge mchanga katika siasa sawa na mdogo wake ambaye naye aligoma kuitwa hivyo akimtaka afute kauli hiyo.
Katibu Msaidizi wa CCM wilayani humo, Bw. Hamis Mkaruka alikiri kupokea taarifa za madiwani hao kutishiana maisha na kutaka kupigana mbele ya Kituo cha Polisi.
Majira lilipowauliza madiwani hao, kila mmoja alikiri kutishiwa maisha na kutaka kupigana mbele ya OCD hivyo walikiomba
chama hicho kitende haki kinapowajadili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment