Na Stella Aron
RAIS Jakaya Kikwete ameeleza kuogopeshwa na kulegalega kwa amani, utulivu na usalama wa nchi hasa katika kipindi cha mwaka jana.
Rais ameomba hali iliyojitokeza mwaka jana basi isijitokeze tena mwaka huu kwani hata alipolazimika kutumia vyombo vya dola bado hali ilikuwa ngumu hata hivyo anaamini kupitia misikitio na makanisa wakiendelea kuwahubiria waumini hali itakuwa shari.
Kutokana na hali hiyo Rais Kikwete ameyataka madhehebu ya dini kurejesha utaratibu wa zamani wa kukutana pamoja mara kwa mara kujadili mahusiano baina yao ili kuepukana na uhasama wa kidini unaoweza kusababisha machafuko makubwa nchini.
Alisema masuala ya audini siku za nyuma hayakuwepo hapa nchini kutokana na viongozi wa madhehebu ya dini kukutaka na kumaliza tofauti zao mapema.
Rais Kikwete alisema hivi sasa utaratibu huo umetoweka hali inayochangia kutokea kwa machafuko ya udini nchini.
Nionavyo mimi ni kuwa kazi aliyoiacha Rais Kikwete ni bora ifafanyiwa kazi na viongozi wa dini zote kwa kurejesha utamaduni wao wa kukutana mara kwa mara na kumaliza tofauti zao.
Kwa hatua hiyo nina imani kuwa mwaka huu hakutaweza kujirudia yale yaliyotokea mwaka jana kuhusiana na suala la dini.
Viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuelimisha waumini wao kuhusiana na suala la amani ya nchi na namna ya kuepuka kujihusisha na migororo inayoweza kuchangia machafuko ya nchi.
Kuendelea kuwa ushirikiano kwa viongozi wa dini kutasaidia kudumisha amani na utulivu nchini kwani mbali ya kuwa na kazi hiyo pia wana kazi ya kuelimisha jamii kuhusiana na kujiepusha na vurugu za udini, matumizi mabaya ya dawa za kulevya, uvivu, biashara ya ukahaba pamoja na kupiga vitendo vya kuomba na kupokea rushwa ili washiriki vema kujiletea maendeleo.
Tanzania ni nchi yenye amani hivyo Watanzania tunapaswa kutokubali kupoteza amani yetu ambayo imetujengea sifa kubwa si katika Bara la Afrika pekee bali ni dunia nzima.
Mwaka mpya umeanza kwa amani na utulivu hivyo ni bora hayo yakazingatiwa katika kipindi hiki cha mwaka huu na kuepuka kutumika kwa masuala ambayo hayatakuwa na faida kwetu na kusababisha vurugu.
Nina imani kuwa kauli alizozitoa Rais Kikwete tutazizingatia na kuzifayia kazi Watanzania wote na kuendelea umoja na amani iliyotawala katika dini zetu.
Ili kuendeleza amani hiyo wote tunapswa kutokubali kurubuniwa na kushiriki kwenye masuala ambayo yatasababisha uvunjifu wa amani na kusababisha wengine kupoteza maisha. Tanzania ina sifa ya watu wake kupendana bila ya kujali dini wala kabila.
Cha msingi ni bora kukawa na ushirikiano mzuri kati ya viongozi wa dini, waumini na polisi ili kunapotokea mtu ama kikundi fulani chenye nia ya kutaka kuvuruga amani yetu taarifa za siri zikatolewa ili kuwabaini wahusika.
Haitakuwa jambo la busara kukaa kimya kunapobainika kuwepo maandalizi ya uvunjwaji wa amani na kukaa kimya bila ya kutoa taarifa iwe kwa viongozi wa dini ama polisi.
Kukaa kimya bila ya kutoa taarifa kunaweza kuibua masuala mengine ambayo si haara kwa taifa bal;i hata kwa familia yako, kwani inapotokea machafuko huwa hakuna ulinzi wa kila nyumba ama mtu fulani.
Tusikubali hata kidogo kufumbia macho masula yanayochochea amani ya nchi yetu ambapo baadhi ya watu wanataka kuisambaratisha kwa kuahidiwa vitu mbalimbali.Inatupasa kuishi maisha ya umoja na ushirikiano bila ya kujali tofauti za dini zetu wala kabila kama ilivyokuwa awali.
Viongozi wa dini pia wanapaswa kuendelea kuwahusia waumini wa dini zao ili kushikamana na watu wengine na kuondoa tofauti zao na kutokubali kununuliwa kwa gharama zozote ili wakubali kuingia katika machafuko.
Hata hivyo ninawaasa Watanzania wenzangu kuwa amani tuliyonayo tusikubali hata siku moja kuipoteza kwani itakuwa nguvu sana kuanza kuirejesha tena na pia idadi kubwa ya wanawake na watoto watapoteza maisha kutokana na sababu mbalimbali.
Mbali ya viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii lakini pia ni vizuri hata tunapokuwa majumbani tukaelimishana kuhusiana na kuwepo kwa suala la amani na anayeonekana kutojali bora akaelimishwa umuhimu wake na kutokubali kurubuniwa ama kununuliwa kwa gharama yeyote ile ambayo baadaye haitakuwa na faida kwake.
Mungu ibariki Tanzania.
0713 574786
USALAMA WA TAIFA WANAMSHAURI NINI RAIS NI VIZURI WASIFANYE KAZI KISIASA AU KUEGEMEA KWENYE MAKUNDI YANAYOASIMIANA BILA HIVYO INAWEKANA KUTOKEA VITA VYENYE HISIA ZA MAKUNDI YANAYOHASIMIANA
ReplyDeleteTatizo kubwa linaloweka "amani/utulivu" wetu majaribuni ni udhaifu na unafiki wa viongozi wetu na kuchangiwa na "partiality" ya majeshi yetu yote. Wanayoyahubiri siyo wanayodhamiria wala kuyatenda! Kila wenye kutafakari,na wenye macho na masikio ...
ReplyDeleteRais na wewe fanya "homework yako". Zipo radio na magazeti ya kidini kazi yake ni kukashifu dini zingine, kutukana viongozi hasa mwasisi wa Taifa letu Mwl Nyerere, kuchochea uhasama kwa Tafsiri potofu za mfumo wa uendeshaji wanchi ukiitwa eti ni mfumo kristo, mihadhara isiyo na tija ya kukosoa imani zingine badala ya kutangaza imani zao, na upuuzi kadha wa kadha. Rais umeviacha kushamiri na kuendelea kuwapotosha maamuma. Ni hawa wasiokuwa nataarifa sahii wanachoma makanisa na kuhatarisha amani yetu. Tuwe specific Rais taja dini gani inaeneza uongo kwa watu na kuharibu mali za wengine, taja Rais maana wanajulikana kuwa ni baadhi ya vikundi vya kiislamu
ReplyDelete