29 January 2013
JK kuzindua mkutano wa TNBC
Na Heri Shaaban
RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuzindua mkutano wa biashara wa Kitaifa Machi mwaka huu, utakaohusu semina elekezi kuhusiana na majadiliano ya ushirikiano kwa wote.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na mtaalam wa mazingira ya kufanya biashara kutoka Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Willy Magehema wakati wa kufungua mafunzo ya siku moja yalioandaliwa na baraza hilo.
Alisema kuwa mkutano huo una lengo la kuwainua Watanzania wenye kipato cha chini wawe na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Madhumuni ya mkutano huo wa majadiliano kuwapa elimu viongozi wa kuanzia ngazi ya mtaa hadi Taifa,kwa kushirikisha Jeshi la Polisi ili elimu hiyo iweze kuwafikia kwa kuwa wanashirikiana na wananchi katika utendaji wa kazi zao.
Pia alisema kuwa lengo kuu kuwapa nyenzo watendaji hao katika kusimamia majukumu yao ambapo mwenye nafasi ndogo kiutendaji awe na uwezo mkubwa kwa ajili ya kukuza uchumi wa Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Temeke Sofia Mgema aliwataka Watendaji wote nchini kusimama na kuangalia uzalendo na kuweka siasa pembeni ili malengo yaliokusudiwa yanatekelezwa kwa manufaa ya Taifa.
Aliwataka Watanzaia kujituma kwa uzalendo katika nyanja za sayansi na teknolojia na kuibua miradi mbalimbali ya ubunifu.
Naye Kamishina wa Kanda Maalum Dar es Salaam Sulemani Kova alisema kuwa bila usalama akutakuwa na uwekezaji mzuri,jeshi la polisi litakikisha linaimalisha ushirikiano ili polisi na raia wawe kitu kimoja katika kukuza uchumi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment