07 January 2013
CHANETA kukutana Jan. 10 kujadili Uchaguzi Mkuu
Na Amina Athuman
CHAMA cha Netoboli Tanzania (CHANETA), kinatarajia kukutana Januari 10, mwaka huu kujadili mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa chama huo uliopangwa kufanyika kati ya Februari na Machi.
Akizungumza mkoani Pwani juzi, Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Bayi alisema fomu za uchaguzi huo zitaanza kutolewa nwishoni mwa mwezi huu na kila kitu kitawekwa wazi baada ya mkutano huo.
Alisema uchaguzi huo ulipangwa kufanyika kati ya Februari na Machi mkoani Dodoma ili kutoa nafasi kwa wanachama wa mkoa huo kuzidi kuhamasisha wakazi wa mkoani humo kuupanda mchezo huo.
"Kama tutapata wafadhili tumepanga uchaguzi huo ufanyike mkoani Dodoma na tumefanya hivyo ili kutoa nafasi kwa wanachama wetu kuandaa matukio muhimu kama mashindano pamoja na mambo mengine," alisema Anna.
Alizitaja nafasi ambazo zitawaniwa katika uchaguzi huo ni uenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini na Mhazini Msaidizi na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.
Aliwataja pia viongozi wanaomaliza muda wao kuwa ni yeye (Anna),Makamu wake, Shyrose Banji, Katibu Mkuu, Ana Kibira (alisimamishwa),Katibu Msaidizi, Rose Nkisi, Mhazini Flora Katambala na wajumbe ni Rose Kisiwa, Fatuma Kisengo, Marry Protas na Damiani Chonya.
Aliongeza kwa kutoa wito kwa wadau wa mchezo huo wenye nia ya dhati ya kuendelea na kuufikisha mbali mchezo huo kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu pindi mchakato wa uchaguzi huo utakapotangazwa rasmi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment