08 January 2013
Afariki kwa kupigwa na radi
Na Lilian Justice,Morogoro
MWANAMKE mmoja mkazi wa Kisaki Kituoni wilayani Morogoro amefariki dunia baada ya kupigwa na radi nyumbani kwake na kufariki dunia papo hapo huku mumewe akipatwa na majeraha .
Akizungumzia kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Bw.Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 5, mwaka huu, majira ya saa 9.30 jioni huko maeneo ya Kisaki katika Tarafa ya Bwakila wilayani humo.
Kamanda Shilogile alimtaja aliyefariki dunia ni Bi.Theresia Gitani (28),mkazi wa Kisaki alifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa na radi akiwa nyumbani kwake huku mumewe Bw.Athuman Abdala akipatwa na majeraha katika tukio hilo.
Aidha alisema mumewe anapatiwa matibabu zaidi katika kituo cha afya cha Duthumi.
Wakati huo huo, mtu asiyefahamika jina lake anayekadiriwa na umri kati ya miaka 25-30 amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akisafiria kuacha njia na kupinduka.
Kamanda Shilogile alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 5, mwaka huu majira ya saa 4.14 as usubuhi huko katika eneo la Misongeni katika Barabara ya Morogoro-Matombo katika Manispaa ya morogoro.
Aidha alisema kuwa gari lenye nambari za usajili T 412 DWM Toyota
ikiendeshwa na Bw. Robert Makarius mkazi wa Misufini mjini hapa
ikitokea Mkuyuni-Mjini hapa iliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha mwanaume ambaye ahakuweza kutambulia jina lake mwenye kukadiriwa kuwa na umri kati ya mika
25-30.
Hata hivyo chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva na mwili wa
marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa ya Morogoro huku mtuhumiwa wa tukio hilo kushikiliwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment