01 August 2012

Kufungiwa Mwanahalisi, Kubenea afunguka *Wahariri watoa tamko zito



Grace Ndossa na Willbroad Mathias

SIKU moja baada ya Serikali kutangaza kulifungia Gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana, MKurugenzi Mtendaji wa gazeti hilo. Bw. Said Kubenea, ameitaka Serikali ifute amri hiyo.

Bw. Kubenea aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema ameshangazwa na kitendo cha Serikali kulifungia gazeti hilo kwani barua waliyopokea, haielezi wamefungiwa kwa kosa gani.

“Serikali inapaswa kuacha kutishia maisha ya raia wake kwa njia  ya kuwaondoa katika biashara na kuwaomba wasomaji pamoja na wadau wa habari, wasimame pamoja kudai haki ya kutafuta na kusambaza habari,” alisema.

Aliongeza kuwa, Serikali imedhamiria kuwatesa wafanyakazi na watendaji wengine wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers inayochapisha gazeti hilo kwa njia ya kulifungia.

“Kufungiwa gazeti hili kunahatarisha maisha ya wafanyakazi, wachapishaji na wauzaji kwani wote, Serikali imeweka misha yao kiganjan,” alisema Bw. Kubenea.

Naye Wakili wa Kampuni hiyo Bw. Rugemeleza Nshala, alisema kampuni hiyo itachukua hatua stahiki baada ya bodi ya Kampuni hiyo kukaa na kujadili kwa kina.

Wakati huo huo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimelaani uamuzi wa Serikali kulifungia gazeti hilo kwa muda usiojulikana.

Kimesema hatua hiyo ni matumizi mabaya ya sheria ya magazeti pamoja na kwenda kinyume na utawala bora.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwenye vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Bw. John Mnyika, imeitaka Serikali kulifungulia gazeti hilo haraka iwekanavyo.

Bw. Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, alisema tayari chama chake  kimewasiliana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na chama hicho kuchukua hatua za kibunge kuisimamia Serikali, kurekebisha udhaifu huo kama itakuwa inaheshimu uhuru wa habari na inazingatia masilahi ya taifa.

“CHADEMA inaitafsiri hatua ya Serikali ya kulifungia gazeti hili ni sawa na kufungia uhuru wa kusambaza habari, kupokea na kutoa maoni hivyo tunatoa mwito kwa wananchi na wadau wote wa habari kuungana pamoja kupinga hatua hii,” alisema Bw. Mnyika.

Alisema chama hicho kitaendelea kuchukua hatua za ziada kama Serikali haitasikiliza kauli za wadau wa habari juu ya suala hili.




3 comments:

  1. UHURU WA HABARI NI MUHIMU SANA LAKINI MASILAHI YA TAIFA NI MUHIMU ZAIDI HATA MARIKANI WANAHANGAIKA KUMWEKA NGUVUNI ALIYEVUJISHA SIRI ZA MAARUFU "WEEKLEAKS" MACHAFUO MENGI DUNIANI NI MATOKEO YA TWEETER NA FACEBOOK KALAMU IKITUMIKA VIZURI HUJENGA ILA IKIUMIKA VIBAYA NI SILAHA YA MLIPUKO HUSABABISHA MAAFA YA KUTISHA YOTE HAYO NI UKOSEFU WA UZALENDO NI UKOSEFU WA MAADILI HAKUNA CHUO CHA MAADILI MBONA HABARI ZA ISRAEL,CUBA AU CHINA ZINAZOZAGAA HUWEZI UKAANDIKA SIRI ZA MKEO AU MUMEO KWENYE MAGAZETI NI UHAYAWANI TUJIREKEBISHE NI ULIMBUKENI WA UHURU WA HABARI MATAIFA MENGINE WANATUCHEKA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ninakubaliana na wewe katika kulinda maslahi ya Taifa na Matumizi mazuri ya kalamu.Lakinindugu yangu Maslahi ya Taifa hayaji kwa kuwaziba watu midomo, Serikali iliyhochaguliwa kidemocrasia ni sharti ichukue hoja za watu makini kama changamoto. Serikali inapojirekebisha baada ya kukosolewa ndio ishara ya kulinda maslahi ya taifa.Ndugu yangu uzalendo ulizikwa na hao walioko madarakani wakati azimio la arusha linawekwa kapuni na kuanzishwa azimio la zanzibar. Kipekee sijasoma habari yeyote inayohatarisha amani katika MwanaHalisi zaidi ya kuutafuta ukweli unaotaka kufichwa, kutetea haki za raia, kutoa elimu ya uraia kwa jamii na kuongeza ufahamu zaidi kwa watanzania.Nihitimishe kwa kupata toka kwako,kwa mfano tu kama wewe unakuwa Dr Ulimboka au ni Baba yako mzazi,ungejihisi vipi kwa hayo yaliyomkuta? unasemaje juu ya Dowansi, Epa, deep green ununuzi wa rada?mauwaji ya Gen Kombe na mengineyo. Yupi kati ya mwanahalisi na Wazimri anazingatia maslahi ya Taifa?Ukweli utabakia ukweli tuwauge wapambanaji mkono tuurejeshe uzalendo uliozikwa.

      Delete
  2. wewe uliyeandika haya inawezekana una vijidudu vya malaria vinavyoshambulia ubungo wako. vema ukapime mapema kabla hata hujapelekwa ICU.mambo ya Israel na cuba yatakusaidia nini kama huwezi pambanua mazuri na mabaya ndani ya Nchi yako mwenyewe. wahi upimwe haraka Medula oblangata isimalizwe na vijidudu vya plasmodium!!!

    ReplyDelete