27 June 2012
Walioficha pesa Uswisi kuchunguzwa
Na Benedict Kaguo, Dodoma
WABUNGE wameitaka Serikali kufanya uchunguzi wa fedha zilizokamatwa nchini Uswisi sh. bilioni 300, kwenye akaunti za Watanzania sita wakiwemo wanasiasa.
Fedha hizo zinadaiwa kuingizwa katika akaunti hizo na Kampuni za uchimbaji mafuta na madini zilizopo nchini.
Mjadala kuhusu fedha hizo, jana ulilitikisa Bunge linaloendelea mjini Dodoma kutokana na hoja za Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA) na Mbunge wa Nkasi, Bw. Ally Kessy (CCM).
Katika mjadala huo, Bw. Kabwe aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), pamoja na vyombo vingine vya usalama, kuwachunguza Watanzania hao na kuwataka majina ili wananchi wawajue.
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona kampuni zinazofanya utafiti wa gesi katika mikoa ya Lindi na Mtwara, zinanunua vyakula kama mchele, mchicha na mafuta ya kupikia mjini Mombasa nchini Kenya badala ya kununua nchini ili kukuza kipato cha wakazi wa mikoa husika.
Aliongeza kuwa ni vyema Serikali ikafanya uchunguzi wa haraka ili Taifa lisiingie aibu katika vita dhidi ya rushwa.
Kwa upande wake, Bw. Kessy alisema ni jambo la kusikitisha kuona watu wameanza kufanya ufisadi katika mikataba ya gesi wakati haijaanza kuchimbwa hivyo wote walioingiziwa fedha hizo watajwe hadharani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hata wakitajwa hadharani itasaidia nini wakati dhamira ya kuwafikisha mahakamani haipo?No accountabilty,sana sana atahamishwa kutoka point A to point B,full stop.Tufanye nini? Tuwaelimishe wananchi ili kwa ujumla wao washiriki uchaguzi wa 2015 na wachague viongozi wenye sifa na wajitokeze sasa kutoa maoni hasa kurudisha madaraka kwa umma.
ReplyDeleteIWAPO KARNE HII WATANZANIA HAINA RASILIMALIWATU YA KUGUNDUA DAWA FEKI JE ANA UWEZO WA KUGUNDUA VYAKULA VILIVYOISHA MUDA WAKE NI NANI ALE SUMU ASIYEJIPENDA WATANZANIA TUFANYE NINI TUNATUMIA KINACHOPATIKANA SIO KINACHOTAKIWA MWILINI
ReplyDelete