25 June 2012
Walalamikia bidhaa kupanda bei kinyemela
Na Salim Nyomolelo
SIKU chache baada ya Serikali kusoma bajeti ya mwaka wa fedha 2012/13 bungeni mjini Dodoma, baadhi ya wafanyabiashara jijini Dar es Salaam, wameanza kupandisha bei ya bidhaa mbalimbali.
Wakilalamikia hali hiyo, baadhi ya wakazi wa jiji hilo walisema kitendo kinachofanywa na wafanyabiashara hao ni kinyume na utaratibu ili kutaka kujinufaisha.
Walisema miongoni mwa bidhaa zilizopandishwa bei kabla ya Julai mosi mwaka huu ni pamoja na sigara ambazo zilikuwa zikiuzwa sh.100 hadi sh.150 pamoja na vinywaji vyenye vilevi.
Akizungumza na Majira, mkazi wa jiji hilo Bw. Festus Swai, alidai kushangazwa na baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bei ya bidhaa kabla muda wake haujafika.
“Baadhi ya maduka ya vinywaji, yameshaanza kuuza bia kwa bei ya sh. 1,900 hadi sh. 2,000 badala ya sh. 1,800, ambayo ndio bei halali ya Serikali kwa sasa,” alisema Bw. Swai.
Naye Bw. Mohamed Issa, aliiomba Serikali kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote wanaopandisha bei ya bidhaa kwa sasa na kusababisha mzigo mkubwa kwa wanunuaji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment