26 June 2012

Waislamu wakubali kushiriki sensa *BAKWATA: Itasaidia kuchochea maendeleo


Na Salim Nyomolelo

BARAZA la Waislamu nchini (BAKWATA), limewataka Waislamu wote kuungana na wananchi wengine kushiriki Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu nchi nzima.

Shekhe Mkuu wa Tanzania, Shaaban Idd Simba alitoa wito huo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko lililotolewa hivi karibuni na Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu linalowataka Waislamu kutoshiriki sensa.

Alisema suala la sensa limekuwa likifanyika nchini mara nyingi bila kuhusisha dini wala ukabila jambo lililozoeleka na kukubalika hivyo kilichojitokeza hivi karibuni ni takwimu za sensa zilizotolewa na watu ambao hawana dhamana hiyo.

“Tunaiomba Serikali itunge sheria ambayo itamtambua mtu ambaye atawajibika kutoa taarifa ya Sensa na Makazi.

“Sensa inaeleweka ni jambo la kisheria na maendeleo katika nchi ila takwimu zilizotolewa na kuainisha idadi ya Waislamu na Wakristo, ndizo zimechangia tatizo lilolopo,” alisema Shekhe Simba.

Aliwataka Waislamu kushiriki sensa kwa ukamilifu, kuwapa ushirikiano wahusika na wasisite kuiomba Serikali iwafafanulie kuhusu takwimu zilizotolewa zikionesha idadi ya Waislamu na Wakristo kama wanataka.

1 comment:

  1. huyo shekh atakuwa amesha kula ki2chochote anataka kutuzingua tu waisilam lakini ipo siku tuta wachoka hawa mashekh ambao wakipew ki2 wana wazunguuka waisilam

    ReplyDelete