27 June 2012
Wafugaji walia njaa Ngorongoro
Na Pamela Mollel, Arusha
JAMII ya wafugaji wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha imeelezwa kutokana na ukosefu mkubwa wa chakula wamefikia hatua ya kuhama ovyo makazi yao.
Pia wananchi hao wameitaka serikali kuwarudishia kilimo chao cha viazi ambacho awali walikuwa wanalima katika Tarafa ya Ngorongoro ili waweze kujikimu katika suala la chakula badala ya kutegemea serikali na chakula chake cha msaada.
Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro ambao ni jamii ya wafugaji (Wamasaai)wameonnesha kukerwa na hali hiyo huku wakiitaka serikali kuchukua hatua za haraka ili kuwanusuru na janga la njaa.
Akizungumza na Majira jana Mwenyekiti wa Kijiji cha Rkeepusi Bw.Tung’ungwa Leyaan alisema, kwa sasa wananchi wamekuwa na hali mbaya hususan ukosefu wa chakula jambo ambalo linawapelekea wao kuhama makazi yao na kwenda mijini ili kutafuta ajira huku ajira nyingine zikiwa si rasmi.
“Wamasai sasa hivi wamekuwa wengi sana hapa mijini, kutokana na ukosefu wa chakula na kama mtu yeyote ana njaa hawezi kukaa lazima atafute sehemu yenye chakula ili aweze kula na hali hii sasa inapelekea wao kuwa walinzi katika nyumba za watu," alisema Mwenyekiti huyo.
Akielezea kwa uchungu juu ya suala la njaa alisema kuwa tatizo hilo ni kubwa na ukizingatia kuwa hawalimi hivyo limekuwa tatizo kubwa kwao kwa kutegemea tu ufugaji.
“Miaka ya nyuma tulikuwa na kilimo cha kujikimu cha kulima viazi na baadaye kuja kusitishwa na serikali kwa madai kuwa hiyo ni sehemu ya hifadhi," alisema.
Katika hilo alihoji serikali iwapo itaweza kuwahudumia kwa chakula cha bure hadi lini huku akisema kuwa hata kama mtu anakupa msaada flani mara kwa mara itafiakia mahali atachoka kutoa msaada huo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment