28 June 2012

Business Times, Jeshi Stars uso kwa uso


Na Elizabeth Mayemba

TIMU ya netiboli ya Business Times LTD, inatarajiwa kucheza Jumapili na timu ya Jeshi Stars katika michuano ya Bandari Chalenji inayotarajia kuanza Jumamosi katika viwanja vya Klabu ya Habours Kurasini, Dar es Salaam.

Timu ambazo zitafungua dimba ni kati ya Bandari A ambao ni wenyeji watacheza na CMTU, ambapo mechi ya pili itakayoanza saa 11 ni kati ya Vijana Barracks na Uhamiaji.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mratibu wa michuano hiyo, George Wakuganda alisema michuano hiyo itakuwa ikifanyika Jumamosi na Jumapili pekee.

"Maandalizi yote yamekamilika hivyo tunatarajia kuanza rasmi michuano hiyo Jumamosi, timu zote zinatakiwa kuzingatia muda kwani muda wa kuanza ni saa 10 jioni," alisema Wakuganda.

Alisema mgeni rasmi katika michuano hiyo atakuwa Mbunge wa Kibaha Mjini Celina Koka.

Wakuganda alisema mechi za Jumapili mbali ya Business Times na Jeshi Stars, mechi nyingine zitakuwa ni kati ya Bandari B watacheza na Kambangwa, Vatican City dhidi ya Maganga Queens.

Alisema jumla ya timu 10 zimethibitisha kushiriki michuano hiyo, ambayo itakuwa katika mtindo wa ligi hatua ya awali, kabla ya kupata timu nne za juu ambazo zitakuwa zimeingia nusu fainali.

Aliongeza kuwa michuano hiyo itasimamiwa na Chama cha Netiboli Mkoa wa Dar es Salaam (CHANEDA). Washindi wa kwanza hadi watatu watapata zawadi nono.

No comments:

Post a Comment