08 May 2012
Makalla ahidi neema katika michezo
Na Grace Ndossa
NAIBU Waziri wa Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni, Amos Makalla amesema changamoto zilizopo kwenye sekta ya michezo atahakikisha anazitafutia ufumbuzi.
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana baada ya kuipishwa kuwa Naibu Waziri katika wizara hiyo na Rais Jakaya Kikwete na kueleza kuwa anatambua changamoto zilizopo katika sekta hiyo
.
"Natambua changamoto zilizopo katika sekta hiyo, hivyo wadau wa michezo wamepata mtu anayefaa katika nafasi hiyo na kuahidi kuchapa kazi kwa kushirikina na wanamichezo,"alisema Makalla.
Aliongeza:"Kwa kuwa mimi ni mwanamichezo nitahakikisha nafasi hiyo naitumia vyema kuimarisha changamoto zinazoikabili sekta hiyo".
Alisema changamoto zilizopo katika sekta hiyo anazitambua na hivyo atazifanyia kazi ili waweze kusonga mbele bila kurudi nyuma.
Hata hivyo, alitamba kuwa anaimudu nafasi aliyochaguliwa kwani kwa kushirikiana na waziri wataangalia changamoto zilizopo katika sekta hiyo na kuzifanyia kazi.
Alisema kuwa wadau wa michezo wakae mkao wa kula kwani hata yeye ni mwana michezo na ni Kapteni wa time ya Wabunge.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkhriZg5qJXBiZD38yaukF105H1Q8MbZOV2K5tB9EUzLVryYlLxL_b3-EItuzfNPM-95aZVYHq8RyG8z5PCusQ5wKg1IOPpgBMzWkIzsPFdC1QhfmEW6wZe9nrMqGZZ-cSLu0aP_aOZTg/s760/times+fm.jpg)
No comments:
Post a Comment