08 May 2012

Azam FC wapongezana kwa mafanikio


Na Victor Mkumbo

WACHEZAJI na viongozi wa klabu ya soka ya Azam FC, wamepewa tuzo na uongozi wa klabu hiyo baada ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara na kushika nafasi ya pili.

Wachezaji hao walipewa tuzo za vyeti baada ya kuonekana kujituma vilivyo katika Ligi Kuu na kuonesha ushindani mkubwa.

Katika hafla hiyo, iliyofanyika Dar es Salaam juzi usiku, mshambuliaji John Bocco alizawadiwa tuzo ya kuwa mfungaji bora wa msimu uliopita baada kufunga mabao 19 ambapo hakuna mchezaji wa timu yoyote aliyofikia idadi hiyo.

Naye Mwenyekiti wa klabu hiyo, Abubakar Bakhresa, alisema wachezaji hao hawana budi kuwa waangalifu katika kipindi hiki cha likizo.

Alisema kwakuwa wametoa mchango mkubwa katika kufanikisha timu hiyo kushika nafasi ya pili, wasibweteke bali waendelee na nidhamu waliyokuwa nayo katika kipindi chote cha msimu uliopita.

Alisema kutokana na mafanikio hayo wanatarajia mwakani kujipanga vizuri na hatimaye kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.




No comments:

Post a Comment