08 May 2012
Kaseba:Siogopi KO ya Cheka
Na Mwali Ibrahim
BINGWA wa mchezo wa Kickboxing nchini, Japhet Kaseba ametamba KO ya Francis Cheka dhidi ya Mada Maugo, haimtii hofu katika pambano lao litakalofanyika Sikukuu ya Sabasaba katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kaseba amejitapa hivyo licha ya pambano lao la mwaka 2009 dhidi ya Cheka kukung'utwa kwa KO ambapo pambano la sasa litakuwa katika uzito wa kilogram 75, raundi 12 huku Cheka akiutetea ubingwa wake wa IBF aliounyakua baada ya kumtwanga Maugo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaseba alisema yeye hatishwi na matokeo hayo zaidi anaendelea na mazoezi ili kuhakikisha katika pambano hilo hafanyi makosa.
"Yale ni matokeo yake na Maugo lakini mimi hayanitishi zaidi ya kunipa changamoto ya kuweza kujiweka sawa na kuweza kumkabili katika mashindano hayo," alisema.
Alisema tayari ameishaanza mazoezi kwa ajili ya pambano katika gym yake iliyopo komakoma, Mwanyamala na ana imani atafanya vyema kwani ana muda mrefu wa kujiandaa.
Alisema katika kipindi chote kabla hajapata pambano alikuwa akifanya mazoezi, hivyo ana imani hadi kufikia siku hiyo atakuwa amepata mazoezi ya kutosha.
.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment