13 March 2012

Utoaji huduma MNH waimarika

Na Rehema Maigala
HALI ya utoaji huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeimarika baada ya madaktari kusitisha mgomo wao kuanzia Jumamisi iliyopita.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, baadhi wagojwa waliokuwepo hospitalini hapo walisema hali ya utoaji huduma imerejea katika hali yake ya kawaida, tofauti na siku mbili za mgomo.

"Kweli hali kwa sasa inalidhisha, kwani siku mbili za mgomo  hali ilikuwa mbaya kiasi cha baadhi ya wagonjwa kukata tamaa," alisema mmoja wa wagonjwa, Stamili Hamisi.

Naye Bw. Hamisi Musa ambaye amelazwa katika wodi ya Kibasila namba tatu kwa sasa hali ni nzuri kwani, madaktari alivyoanza mgomo ndugu zake walimpeleka katika hospitali nyingine.

" Ndugu walinirudisha Muhimbili baada ya mgomo kumalizika nashukuru madaktari wanaendelea kutupa huduma kama ilivyo mwanzo," alisema.
Kwa upande wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), hali wagonjwa walikuwa wengine wakiendelea kupata.

Akizungumza na gazeti hili Ofisa Uhusiano wa MOI, Bi. Mery Ochieng, alisema kwa sasa huduma zinaendelea kama kawaida na wanawataka wagonjwa waliopangiwa siku za mazoezi kufika bila kukosa.

No comments:

Post a Comment