Na Israel Mwaisaka
BAADHI ya wazee na madiwani katika Halmashauri ya Wilaya Kyela mkoani Mbeya wameazimia kuunda Tume itakayokwenda kuonana na Rais Jakaya Kikwete ili kutaka kujua tatizo la ugonjwa anaougua Mbunge wa Kyela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Dkt.Harrison Mwakyembe.
Azimio hilo lilifikiwa mwishoni
mwa wiki na wazee hao kufuatia mkutano wa hadhara uliokuwa umeitishwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kyela Mjini, Bw.Gabriel Kipija ambapo moja kati ya ajenda za mkutano huo ilikuwa ni kutaka kuishinikiza Serikali kueleza uwazi wa ugonjwa unaomsumbua Dkt.Mwakyembe.
Kwa madai ni kutokana na kutokea kwa mkanganyiko kwa baadhi ya watendaji wa Serikali juu ya ugonjwa unaomsumbua Mbunge wao. Akizungumza katika kikao hicho Mzee Benson Mwaikeke alisema, ni jambo la kushangaza kuona Serikali inakuwa na taarifa zinazokinzana miongoni mwa watendaji wake. Alisema, taarifa ya Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba ambayo i l i tolewa awali kuwa Dkt . Mwakyembe hakulishwa sumu imekinzana na taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw.Vuai Nahodha ikiwa ni pamoja na ile ya Waziri wa Afya, Dkt.Mponda. Alisema, kitendo hicho cha Dkt.Mwakyembe kuugua na kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Kimataifa Apollo nchini India wao kama watu wa Kyela wameumia kiasi kikubwa hivyo wanaposikia taarifa zinazokinzana juu ya ugonjwa huo kati ya viongozi hao wa Serikali ni bora sasa wakaonane na Rais Kikwete ili aweze kubeba dhamana ya kuwaambia wananchi juu ya kile kinachomsumbua Dkt. Mwakyembe.
Diwani wa Kata ya Bujonde Bw.Lameck Mwambafula kwa upande wake alisema, ipo haja sasa kwa Rais ya kuhakikisha anamfukuza kazi DCI Manumba kutokana na taarifa yake ambayo anadai kuupotosha umma na kutaka kuuficha ukweli uliopo katika suala zima la kinachomsumbua mbunge wao na kuwa kutokana na hilo DCI Manumba amekosa sifa ya kuwa mtumishi ndani ya Serikali. Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi wilayani Kyela Bw. Robinson Fongo alisema, umefika wakati kwa jamii sasa kuhakikisha kuwa wanafanya maandamano ya amani yatakayoishinikiza Serikali kuweza kutoa taarifa sahihi na kuachana na ubabaishaji uliopo kati ya watendaji wa Serikali. Alidai, suala hilo peke yake linaonesha ni jinsi gani viongozi wa nchi wasivyokuwa pamoja na kufanya kazi kama timu hali inayopelekea kila mmoja kuzungumza anavyotaka yeye.
A l i s e m a , h a r i h i y o hawataweza kupata taarifa sahihi za kinachomsumbua Dkt.Mwakyembe kwa kuwa viongozi wote wa Serikali kila mmoja anatamka atakavyo yeye na kuacha maadili ya yanayowaongoza kwenye utumishi wa umma na kuwa njia pekee ni maandamano tu na kuunda Tume ya watu kwenda kumwona Rais na kumpelekea ujumbe huo wa watu wa Kyela. Hata hivyo Mwenyekiti huyo
wa halmashauri, Bw.Kipija alisema, hoja hiyo wataifanyia kazi haraka na kuunda tume ambayo itawashirikisha watu mbalimbali wa wilaya hiyo bila ya kujali itikadi za kisiasa kwani lengo ni kutaka kuunda umoja utakaoweza kumfikishia taarifa Rais Jakaya Kikwete. Alisema, licha ya hoja hiyo pia watazingatia ushauri uliotolewa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bw.Fongo ya kutaka kuitishwa kwa maandamano ya amani ili kuonyesha umma wa Watanzania kuwa sasa wamechoshwa na ubabaishaji unaofanywa na viongozi waliopo madarakani.
hee loli mujobile bandu bha Kyala, ndo watajua kwamba kyela si pa mchezo na salaamu kwa lowassa na kundi lake.
ReplyDelete