05 March 2012

Simba ni raha kwenda mbele

  • Yaifurusha kiyovu CAF
  • Mashabiki wang'oa viti                                                                                                                       Na Elizabeth Mayemba
    WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho (CAF), Simba wanashuka Uwanja wa Taifa leo kucheza na Kiyovu ya Rwanda katika mchezo wao wa marudiano wa kombe hilo.

    Katika mchezo wao wa kwanza uliochezwa Februari 18 mwkaa huu,timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.Mchezo huo ulichezwa mjini Kigali,Rwanda.

    Simba leo wanahitaji sare ya aina yoyote ile ili waweze kusonga mbele, kutokana na faida ya bao moja la ugenini.

    Macho na masikio ya Watanzania leo hasa wale mashabiki wa Simba yatakuwa kwa timu yao kuona itavuna nini katika michuano hiyo, kwani endapo watakubali kufungwa watakuwa wameiaga rasmi michuano hiyo.

    Akizungumzia mchezo wa leo Kocha Mkuu wa Wekundu hao, Milovan Cirkovic alisema kurudi uwanjani kwa kiungo wake Haruna Moshi 'Boban' aliyekuwa majeruhi na hivyo kuukosa mchezo wa kwanza kutaisaidia sana safu ya ushambuliaji.

    "Nina wachezaji wazuri sana katika kikosi changu, lakini pia kurudi kwa kiungo wangu Boban kutaongeza nguvu katika kikosi changu, hivyo safu ya ushambuliaji itakuwa imara kwani Boban kwa kushirikiana na kiungo mwenzake Mwinyi Kazimoto watakuwa wakiirahisishia safu ya ushambuliaji," alisema MKilovan.

    Alisema wana kila sababu ya kushinda mchezo wa leo, hasa kutokana na matokeo ya ugenini pia wachezaji wake watakuwa wakicheza mbele ya mashabiki wao, ambao watakuwa wakiwapa morali kutokana na ushangiliaji wao.

    Mshindi atakayepenya leo, atakutana na timu ya ES Setif ya Algeria.

    ends......


No comments:

Post a Comment