05 March 2012

Propaganda za CHADEMA zaleta mageuzi Iringa

Na Eliasa Ally,
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Manispaa ya Iringa mkoani Iringa kimekusanya wanachama wapya 210 kutoka CCM, TLP na CUF baada ya Mbunge wa Jimbo la Iringa
Mjini,


 Mchungaji Peter Msigwa kufanya mikutano mitatu na wananchi kuvutiwa na sera za CHADEMA hivyo kuamua kujiunga kwa hiari.Wananchi ambao walijiunga na CHADEMA ni wale ambao ni wakazi wa maeneo ya Semtema, Soko Kuu la Mkoa wa Iringa na Ipogolo ambapo walijiunga katika mikutano ya hadhara baada ya Mchungaji Msigwa kuwafafanulia kwa kina malengo na dhamira ya chama hicho kupitia mikakati ya kuwakomboa kiuchumi. Katika mikutano hiyo ambayo ilifanyika kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki, Manispaa ya Iringa Mbunge huyo katika eneo la Semtema aliwapata wanachama wapya 72, eneo la Sokoni wanachama wapya 78 na katika eneo la Ipogolo walipatikana wanachama wapya 60. Mchungaji Msigwa akihutubia wananchi hao alisema, chama chake kimeweka dira ambayo inalenga kuwakomboa wananchi katika nyanja zao za maisha na kuongeza kuwa wananchi ambao wamejiunga na CHADEMA hawajakosea wamekwenda mahali sahihi.
Aliongeza kuwa CHADEMA, siku zote kimekuwa kikifanya kila linalowezekana kuwaelimisha wananchi na kuwaeleza ukweli halisi wa haki zao za kimsingi na kuongeza kuwa chama hicho kipo kwa malengo ya kuhakikisha kuwa kinapambana ili kuhakikisha kuwa kinamkomboa mwananchi k u t o k a k a t i k a ma z i n g i r a anayoishi kiuchumi, kiutawala na kimasilahi.
Alizitaja baadhi ya juhudi ambazo chama hicho kimefanya katika Jimbo la Iringa Mjini kuwa ni pamoja na kuwatetea wafanyabiashara, wajasiriamali ambao walikuwa wanauza bidhaa zao eneo la Mashine Tatu. Jitihada ambazo alisema ni baada ya Serikali kuwataka wahamie Semtema mbali na wateja wao na kuongeza kuwa CHADEMA wa t a h a k i k i s h a manufaa ya kwanza anayapata mwananchi. A l i s e m a , C H A D EMA wamefanikiwa kusimamia shughuli za maendeleo ikiwemo kusimamia na kutoa vitanda vyenye thamani ya sh. milioni 60 katika Hospitali ya Muungano, kuhakikisha ujenzi wa barabara ya lami toka
mjini hadi ilipo hospitali hiyo inajengwa, kufufua michezo kwa vijana ambayo ilitetereka awali na kutetea haki za wananchi.

No comments:

Post a Comment