Muonekano wa mkate huo
Na Godfrey Ismaely
UTAFITI umeendelea kubainisha kuwa ulaji wa mikate meupe kupita kiasi umeanza kuwa kikolezo cha kuchochea vifo kwa wingi hususan kuongeza ugonjwa wa saratani pamoja na kisukari.
Kwa mujibu wa utafiti ambao ulifanywa hivi karibuni na wataalamu kutoka nchini Uingereza na baadaye nchini Uswiss ambao umefikia hatua hadi vizuizi vimeanza kuwekwa kwa viwanda vinavyotengeneza mikate hiyo, ulibainisha kuwa maelfu ya watu wamekuwa wakifariki dunia kila mwaka kutokana na ulaji huo.
“Mfano kwa wale ambao huwa wanakula silesi tano kila siku wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya kibofu kuliko wale wenzetu ambao huwa wanakula silesi moja na nusu kwa siku,” ilieleza sehemu ya utafiti huo ambayo iliripotiwa na gazeti la Daily Mail kutoka Uingereza.
Hata hivyo wanasayansi wamebainisha kuwa ulaji huo wa mikate meupe ni hatari zaidi hivyo wakapendekeza kuwa ni bora sasa kila mmoja akaanza kutoa kipaumbele kwa mikate ambayo haijachanganywa na kitu chochote wakimaanisha ngano ambayo haijakobolewa.
Wanasayansi hao walisema kuwa, madhara hayo ambayo yalitokana na mchanganyiko wa kemikali mbalimbali ambazo licha ya kuua viini lishe pia husababisha kupoteza ladha halisi hivyo, kufikia hatua ya kuziba mirija ya damu hadi kusababisha saratani kuendelea kukua taratibu hadi kifo.
“Umefika wakati sasa kila mtu kubadili tabia ya kula mikate meupe ambayo inasababisha ongezeko kubwa la kupanda kwa sukari, kwa kuwa kufanya hivyo ni hiari ya kila mmoja wetu,” ulifafanua utafiti huo.
Pia utafiti huo uliongeza kuwa Serikali ya Uswiss imejiwekea mkakati wa kusitisha ulaji wa mikate meupe kwa raia wake mara baada ya kugundua kuwa imekuwa ikiwasababishia madhara mbalimbali kiafya hususan ugonjwa wa kisukari.
Kwa msingi huo tafiti zinaonesha kuwa Serikali hiyo imeamua kuongeza kiwango kikubwa cha utozaji wa kodi katika viwanda vya uokaji wa mikate meupe ili kupunguza idadi ya walaji.
Wakati makusanyo ya kodi hizo yatakuwa yanatumika kuendelea kutoa elimu kwa umma na kuvisaidia viwanda ambavyo huwa vinatengeneza mikate ambayo ngano yake haijakobolewa ili wananchi wake waweze kuinunua kwa wingi kwa ajili ya matumizi ya chakula na kifungua kinywa nchini humo.
“Hatua hiyo inaenda sambamba na kuepuka kula vyakula vilivyosindikwa kama mikate hiyo ambayo imeokwa baada ya kukobolewa hivyo kupoteza uthamani wake,”uliongeza.
Hata hivyo kwa mujibu wa utafiti mwingine ambao uliripotiwa hivi karibuni na kuchapwa katika Jarida la International Journal of Cancer uliainisha kuwa ulaji huo wa mikate meupe umekuwa kichocheo kikubwa cha saratani.
“Inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya kesi ambazo ziliripotiwa 6,000 zinahusiana na saratani ya kibofu nchini Uingereza kila mwaka, walalamikaji zaidi ya 3,400 wamekuwa wakiathirika kwa kiasi kikubwa na ulaji huo,”
Chuo cha Pharmacological Research kilichopo mjini Milan nchini Italy kilibainisha kuwa Waitaliano 2,300 kati ya hao 1,767 walikuwa na saratani mara baada ya kula mikate hiyo, lakini zaidi ya 1,534 walikuwa katika hali mbaya zaidi baada ya kufululiza kula mikate hiyo kwa miaka miwili.
Wanasayansi waligundua kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya kula mikate meupe kwa wingi na madhara ya kupata ugonjwa wa saratani kwa muda mfupi.
Aidha, watu ambao wapo katika makundi ambayo ula mikate meupe zaidi ambapo kila mmoja ufikisha zaidi ya silesi 35 kwa juma moja ama siku tano wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupata saratani kuliko wale ambao ulaji wao wa mikate hiyo unafikia silesi 11 kwa juma wakimaanisha kula silesi moja na nusu kwa siku.
Hata hivyo utafiti huo unabainisha kuwa ili kuyaweka mambo sawa walaji wa nyama safi na mboga mboga ni bora zaidi kuliko kula mikate hiyo kwa kuwa wapo katika uwezekano mdogo wa kupata saratani hiyo ya kibofu.
“Ingawa baadhi ya tafiti zimekuwa zikikinzana kwa hili, utafiti wetu haukuweza kubainisha wazi kwamba ni aina gani ya mikate inapaswa kulaumiwa zaidi, ijapokuwa watafiti wanaamini kuwa mikate meupe ni dosari kubwa zaidi kwa afya ya mlaji tofauti na mikate ya ngano halisi ambayo haijakobolewa,” ilifafanua sehemu ya utafiti huo.
Mbali na hayo utafiti huo ulibainisha kuwa matumizi ya vyakula ambavyo vimekobolewa yanasababisha na hata kuchochea ugonjwa wa kisukari ambao ufikia hatua ya kusababisha kongosho kuharibika hadi kifo.
“Dhana halisi ni kwamba saratani hiyo huwa inashambulia katika chembe chembe za damu ambazo hutumia vilainisho vya sukari ili kukamilisha kazi yake ipasavyo katika mwili, lakini kutokana na hali hiyo hukwamisha shughuli zote hadi kufikia hatua ya kufifisha shughuli zote na matokeo yake kusababisha hatari katika mwili,” uliongeza.
Kwa mujibu wa mtafiti mmoja, Dkt.Francesca Bravi anasema, utafiti kama huo unapendekeza kuwa ni vyema watu wakaepuka kula vyakula ambavyo havina nafaka zake za asili ikiwemo kuongeza matumizi ya mboga za majani kwa wingi kwa kuwa wanaweza kuziweka afya zao katika hali salama.
“Ndiyo maana katika msingi mzima wa utafiti wetu pia tunapendekeza watu wapunguze ama waachane kabisa na matumizi ya vyakula vilivyokobolewa na kama hivyo mikate meupe na kula vyakula ambavyo vinatokana na nafaka halisi, vikiwa havijabadilishwa kitu chochote,” anasema daktari huyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa tafiti za nyuma zinabainisha kuwa wanawake ambao huwa wanatumia vyakula vyenye viini lishe kamili wapo katika mazingira salama zaidi ya kuepukana na ugonjwa wa saratani ya matiti kuliko wale ambao huwa wanakula zaidi vyakula ambavyo vimekobolewa kama mikate meupe.
Kizuizi cha mikate
Mkate mweupe waongeza idadi ya vifo duniani
Serikali ya Uswiss imejiwekea mkakati wa kusitisha ulaji wa mikate meupe kwa raia wake mara baada ya kugundua kuwa imekuwa ikiwasababishia madhara mbalimbali ya kiafya hususan ugonjwa wa kisukari.
Tafiti zinaonesha kuwa Serikali hiyo imeamua kuongeza kiwango kikubwa cha utozaji wa kodi katika viwanda vya uokaji wa mikate meupe ili kupunguza idadi ya walaji.
Hata hivyo kwa mujibu wa nchi hiyo makusanyo ya kodi hizo yatakuwa yanatumika kuendelea kutoa elimu kwa umma na kuvisaidia viwanda ambavyo huwa vinatengeneza mikate ambayo ngano yake haijakobolewa ili wananchi wake waweze kuinunua kwa wingi kwa ajili ya matumizi ya chakula na kifungua kinywa.
Hatua hiyo inakuja zikiwa zimepita siku kadhaa mara baada ya Serikali ya Canada kupitisha Sheria ya kuzuia matumizi ya mikate meupe ambayo tayari imeondolewa viini lishe vyake na kusisitiza kuwa mikate ni lazima iwe na viini lishe vya asili na si vya kuongezewa kama inavyofanyika hivi sasa.
Utafiti huo ambao ulitolewa hivi karibuni na Uswiss ulifafanua kuwa kiasilia mkate mweupe ni hatari kwa afya lakini jambo la kushangaza wasambazaji na watengenezaji wamekuwa hawataki kuelezea ukweli kuhusiana na madhara yake kwa umma.
“Kimsingi unaweza kutamka wazi kuwa walaji wa mkate mweupe ni ‘wafu’. Mkate watengenezaji na wauzaji wao wanachotafuta ni fedha kwa ajili ya utajiri Je? mlaji yeye utajiri wake utaishia kwenye kifo. Kwa nini? Mikate ni ya rangi nyeupe wakati unga wa ngano si mweupe ukiusaga;
“Ni kutokana na unga huo kuchanganywa na rangi za kemikali kama zilivyo nguo zako zinavyotengenezwa kiwandani, hivyo unavyozidi kula mkate huo wakati unafurahia ladha vivyo hivyo na kemikali inaendelea kukuathiri,” ilifafanua sehemu ya utafiti ambao ulifanywa nchini Uswiss hivi karibuni.
Hata hivyo utafiti huo ulifafanua kwa kina kuwa unga unaotumika kutengenezea mikate hiyo meupe hadi kufikia hatua Uswiss wakaamua kuweka kizuizi imekuwa ikichanganywa na kemikali mbalimbali zikiwemo oxide ya nitrojeni, klorini nitrosyl, hidrojeni na peroksidi ambayo huwa inachanganywa pia na chumvi za kemikali mbalimbali wakati wa maandalizi.
Utafiti huo haukusita kuweka mambo wazi kuwa utayarishaji wa mikate meupe umekuwa ukipitia hatua ambazo bila mlaji ambaye ni mwananchi wa kawaida kuelimishwa madhara yanaweza kuwa makubwa na wakati mwingine wataendelea kupoteza maisha.
“Lakini hapa si hadithi katika
IPO KAZI KWENYE HILI ASEE
ReplyDeleteAhsante kwa taarifa nzuri kwa afya zetu
ReplyDelete