06 March 2012

Mapinduzi ya kilimo chenye tija yanaanzia kwa wakulima

Na Salim Nyomolelo
ZAIDI ya asilimia 80 ya Watanzania tafiti zinaonesha kuwa wanategemea kilimo kwa kuendesha maisha yao ya kila siku hususan kujipatia chakula na kipato.



Mbali na hayo tafiti mbalimbali zinabainisha kuwa idadi kubwa ya Watanzania hao wanategemea kilimo kwa ajili ya kuzalishia mazao ya biashara ambayo yanakuwa na uhitaji mkubwa katika soko la ndani na nje.
Licha ya wananchi kutegemea sekta ya kilimo kwa hali na mali lakini Serikali imekuwa ikiweka mkazo katika kuhakikisha kuwa kilimo kinafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Katika kuhakikisha kilimo kinapewa kipaumbele Rais Jakaya Kikwete anasema kuna haja ya kutumia sayansi na teknolojia katika shughuli za kilimo ambapo Mabwana na Mabibi shamba wanatakiwa kuwafundisha taratibu za kilimo chenye tija vijijini.
Rais Kikwete anasema, ili kuhakikisha sekta ya kilimo inafanikiwa Serikali inafanya mapinduzi ya kilimo pamoja na kuwawezesha wakulima wadogo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula pamoja na kupata soko la uhakika.
Anasema, asilimia 95 ya mazao ya kilimo hutumiwa kwa ajili ya chakula, asilimia 34 kusaidia
Mapinduzi ya kilimo chenye
tija yanaanzia kwa wakulimakupata fedha za kigeni baada ya kuuzwa ambapo asilimia 24 ni kwa ajili ya pato la Taifa.
“Licha ya asilimia zaidi ya 80 ya Watanzania wanategemea katika kilimo, lakini pia asilimia 70 hadi 80 ya watu barani Afrika wanategemea kilimo kwa ajili ya kuendesha maisha yao,” anasema Rais Jakaya Kikwete baada ya kukutana na wadau wa kilimo Ikulu.
Rais Kikwete anasema, kuna haja kubwa ya wakulima kuondokana na matumizi ya jembe la mkono ambalo halimsaidii mkulima mdogo kuandaa sehemu kubwa ya shamba na badala yake kuanza kutumia zana za kilimo za kisasa kama trekta la kukokotwa kwa mikono yaani power tiller.
Anasema, umefika wakati ambapo wakulima nchini wanatakiwa kutumia kilimo cha umwagiliaji maji ili kuepukana na kutegemea mvua ambazo zimekuwa hazina uhakika jambo ambalo husababisha wakulima kukosa mazao baada ya kukauka kwa kukosa mvua muda mrefu.
“Mara nyingi mvua za Mwenyenzi Mungu hazina uhakika jambo ambalo linafanya kilimo chetu kuwa cha kubahatisha na ili kuepukana na hali hii kuna haja kuanzia sasa kutumia kilimo cha umwagiliaji, kwa kuwa nchi yetu imebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji,”anasema Rais Kikwete
Anasema, wakulima wanatakiwa kuwa na matumizi mazuri ya pembejeo za kilimo ambapo matumizi ya mbegu bora yatasaidia wakulima kuvuna mazao mengi.
Rais Kikwete anasema Serikali itahakikisha inaboresha miundombinu ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kwenda vijijini na mazao sokoni.
Anasema, wakulima watapewa hati miliki ya mashamba yao ili waweze kukopesheka na hivyo mikopo itawasaidia katika kuendeleza kilimo ikiwa ni pamoja na kununua zana za kisasa zikiwemo kilimo pamoja na pembejeo.
Rais Kikwete, anasema kwa kuanzia Serikali itatoa mikopo kwa wakulima wadogo wa mahindi katika mikoa ya Iringa, Morogoro, Rukwa, Ruvuma, Kigoma na Mbeya kwa kuwa ndio inayoongoza katika kuzalisha mazao mengi ya jamii hiyo.
“Mikoa hiyo ndio inatusaidia katika kuzalisha mahindi kwa wingi ambapo hutusaidia pia katika kutoa msaada kwa ndugu zetu wa jirani pale wanapokuwa wakikabiliwa na janga la njaa,”anasema Rais.
Anasema, Serikali itaongeza bajeti kwa asilimia 10 kwa mwaka 2012/2013 lengo likiwa ni kukuza mpango wa kilimo nchini.
“Serikali imekuwa ikitathmini sekta ya kilimo na hivyo kila mwaka huwa inaongezewa bajeti ili kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na chakula cha kutosha na kuepukana na janga la njaa,” anasema.
Rais Kikwete, anasema kuwa mwaka 2005 bajeti katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ilikuwa sh.bilioni 236 ambapo iliongezeka hadi kufikia sh.bilioni 926 kwa mwaka 2010.
“Ongezeko hilo la asilimia 10 litasaidia katika kuhakikisha sekta ya kilimo inafanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuleta mavuno mengi yatayotusaidia kuwa na soko la uhakika,”anasema Rais Kikwete.

No comments:

Post a Comment