06 March 2012

Maandamano ya waandishi Iringa yapewa baraka leo

Na Mwandishi Maalum, JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa limebariki maandamano ya waandishi wa habari ambayo yanafanyika leo kwa ajili ya kushinikiza Serikali mkoani humo kutambua nafasi yao na hata kuwashirikisha katika masuala mbalimbali ya jamii. Awali kabla ya waandishi hao kupewa kibali na jeshi hilo lilikutana na Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa (IPC), Bw.Frank Leonard ili kufanya marekebisho ya njia.


Hata hivyo walikubaliana kuifuta njia ya Uhindini na badala yake kuruhusu maandamano hayo kutumia barabara ya Uhuru kutoka Bustani ya Manispaa ya Iringa kwenda Barabara ya Samora hadi Mshindo. Pia waandishi hao baada ya hapo walitakiwa kurudi kwa kupitia Barabara ya Mashine Tatu, Stendi Kuu hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Katika hatua nyingine barua hiyo ya Jeshi la Polisi ambayo liwaruhusu kuandamana leo, ili kuwasilisha mapendekezo yao ilikuwa na kumbukumbu namba IRI/A./14/VOl.x11/178 iliyotumwa kwa Mtendaji Mkuu wa IPC ikiwa na kichwa cha habari 'maombi ya kibali cha kufanya maandamano ya amani'. "Tafadhali rejea barua yako kumb.IPC/02/o12/ ya 03/03/2012 inayohusu kichwa cha habari hapo juu. Kibali kimetolewa cha kufanya maandamano ya amani kwa Klabu ya Wanahabari Mkoa wa Iringa mnamo tarehe 6/3/2012 muda wa saa 4 asubuhi kama ifuatavyo, maandamano hayo yataanzia kwenye Bustani ya Manispaa ya Iringa kuelekea Kanisa la Mshindo kwa kupitia Barabara ya Uhuru; "Baada ya kufika Kanisa la Mshindo watapita barabara ya Ubena Club kuelekea Stendi Kuu ,MR Hotel, Luxury hadi ofisi za mkuu wa mkoa ambapo yataishia. Nakala kwa RPC Iringa kwa taarifa na RTO tafadhali panga askari wa kuongoza maandamano hayo nawatakia maandamano mema Mkuu wa Polisi Wilaya ya Iringa Mohamed Mkwazu Semunyu," ilifafanua sehemu ya barua hiyo. Hata hivyo jana Mkuu wa

Mkoa wa Iringa, Dkt.Christina Ishengoma ambaye alipaswa kupokea maandamano hayo, alikutana bila kufikia makubaliano na wawakilishi wa waandishi hao katika kikao kilichofanyika
mkoani humo. Wakati huo huo Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya (MBPC) kimepongeza
hatua za IPC kutangaza maandamano ya kupinga manyanyaso wanayofanyiwa na Serikali na kuwa wao pia
wapo pamoja na wanahabari hao kupinga hali hiyo. Kat i ka salamu zake z a kupongeza uamuzi huo uliofikiwa na IPC Mwenyekiti wa MBPC, Bw.Christopher Nyanyembe alisema umefika wakati sasa kila idara na ofisi zote za umma zikiwemo binafsi kutoa ushirikiano wa karibu kwa waandishi wa habari ili taarifa sahihi ziweze kuwafikia wananchi kwa wakati.

No comments:

Post a Comment