Na David John
WAATHIRIKA wa mafuliko waliohamishiwa eneo la Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wametakiwa kulinda na kusimamia miundombinu ambayo Serikali imewajengea.
Mwito huo ulitolewa jana na baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam, wakati wakitoa maoni yao kuhusu watu waliohamishiwa eneo hilo baada ya kutokea mafuriko mwishoni mwa mwaka jana na watu zaidi ya 40 kupoteza maisha.
Bw. Henry Makelele ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa visima vya majia alisema ni vema wananchi hao wakawa na uchungu na fedha za umma kwa kutunza mazingira.
Bw. Makelele ambaye amepewa jukumu la kuweka miundombinu ya maji katika eneo hilo alisema; "Pesa nyingi zimetumika kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanapata makazi pamoja na kuwawekea mazingira katika hali mazuri, hivyo ni jukumu lao kuyatunza," alisema
Alisema fedha nyingi zimetumika kukabiliana na hali hiyo, lakini kuna Watanzania wengi ambao wamechangia wezao kukabiliana na shida waliyokuwa nayo.
Aliongeza kuwa serikali imejitahidi kuhakikisha wananchi hao wanapata huduma muhimu kama vile maji , barabara, hospitali na nyingine.
Alisema tatizo kubwa la Watanzania wanakuwa si waangalifu wa mali zao na pindi matatizo yanapotokea wanakuwa wepesi wa kulaumu Serikali.
Naye Bw. Frank Danieli alitoa rai kwa baadhi ya Watanzania ambao bado wanang'ang'ania kuishi mabondeni kuhama katika maeneo hayo ili kuepuka madhara kama yaaliyotokea.
No comments:
Post a Comment