19 March 2012

Kesi ya wapangaji NIC Machi 21

Na Mwandishi Wetu
KESI namba 21/2011 iliyofunguliwa na wapangaji katika nyumba za Shirika la Bima la Taifa (NIC), zilizopo Masaki barabaara ya Chole na Mikocheni B, Dar es Salaam, imepangwa kutajwa Machi 21 mwaka huu, mbele ya Jaji Lugazia wa Mahakama Kuu Divisheni ya ardhi.
Kesi hiyo ilitajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Juni 7,2011 ambapo wapangaji wa nyumba za shirika hilo walitishiwa kuondolewa na mmiliki NIC inayodai kuuza nyumba hizo kwa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)

Hata hivyo, baadhi ya wapangaji katika nyumba hizo waliondoka bila kupinga wengine wakipigana kufa na kupona hadi kile walichoita haki yao ya kuishi muda mrefu ithaminiwe.

Wapangaji hao wansema kuwa, mwaka 2008 Rais Jakaya Kikwete akiwa mkoani Iringa, alisema nyumba za Serikali zilizopo kwenye mpango wa kuuzwa, kipaumbele kitolewe kwa watu walioishi muda mrefu katika nyumba hizo.

Badhi ya vigogo wa Serikali ni miongoni mwa wapangaji katika nyumba hizo ambao hawamo kwenye kesi ya kupinga kuondolewa na kuuzwa kwa nyumba hizo bila kupewa kipaumbele wakidai uwezo wa kuzinunua wanao kama ilivyofanyika kwa nyumba nyingine zilizokuwa zikimilikiwa na Serikali.

Hata hivyo taarifa zilizolifikia gazeti hili zinasema kuwa juzi Jumatatu iliyopita Luhanjo alituma mmoja wa vijana wake kufungua makufuli ya nyumba yake na kufanya usafi hali inayoashiria kuwa anataka kurejea kuanza kuishi.

Wapangaji hao wanatetewa na wakili Bw. Arafat Sinare wa Kampuni ya Law Associates Advocates ya Dar es Salaam, ambaye alifanikiwa kupata zuio la mahakama ili wateja wake wasiondolewe kwa nguvu hadi mahakama itakaposikiliza madai yao.





No comments:

Post a Comment