27 February 2012

Waziri Malima timiza ahadi yako

Mhariri Majira,
UMEFIKA wakati sasa mwananchi anayeonja ugumu wa maisha kupinga kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania.


Ndugu Waziri, sisi wananchi wa mji wa Makambako hasa maeneo ya Uhuru na mizani tumeikosa huduma ya umeme kwa mwezi mmoja na nisu kutokana na transfoma kupata shoti. Naibu waziri, Adamu Malima alipita mwanzoni mwa mwezi wa kwanza 2012, na kufanya mizunguko katika vitongoji na kata za hapa na kujionea hali halisi jinsi tunavyopata adha ya umeme.

Kutokana na hali hiyo, alifanya mkutano na wananchi juu ya suala la umeme na mambo mengine kama gharama za uingizaji umeme majumbani, bei ya nguzo kuwa juu na rushwa katika huduma ya kuingizwa umeme kwa mteja pamoja na mambo mengine juu ya huduma ya TANESCO. Cha kushangaza, pamoja na ahadi nzuri ya waziri na maneno ya kujisafisha aliyotoa Meneja wa TANESCO kuwa atamaliza tatizo hilo, mpaka sasa wananchi wa maeneo ya Uhuru na Mizani hatujui kama shirika hilo linajua matatizo tunayopata. Ndugu waziri kumbuka makofi tuliyokupigia ulipoahidi kutatua tatizo hilo, iweje usahau kufuatilia tatizo letu. Tunaomba umeme tuendelee na ujenzi wa taifa. Mwananchi mpenda maendeleo Makambako.

No comments:

Post a Comment