27 February 2012

Siku 1,000 za kufufua matumaini ya maisha bora kwa Watanzania

Na Mwandishi wetu
TA N Z A N I A n i mi o n g o n i mwa ma t a i f a y a n a y o s i f i k a kwa kuwa kisima c h a a m a n i . Mataifa mengi y a n a i t a z ama kwa jicho la husuda kutokana na
hali hiyo.


Ni taifa lenye makabila zaidi ya 121 wanaopendana na kuishi kwa udugu. Kizuri zaidi wanaunganishwa na lugha ya Kiswahili. Amani iliyopo nchini leo, ina misingi yake, hivyo inatakiwa kuenziwa kwa gharama zote. Tunapoenzi amani hii, ni lazima tutambue mchango wa viongozi wa dini ambao ndiyo chachu ya amani hiyo. Hatuwezi kusema ni matokeo ya vyombo vya usalama peke yake.
Na sema hivyo, kwa sababu ya kutambua kuwa viongozi wa dini, ndiyo msingi wa upendo. Ndiyo maana viongozi wetu wamekuwa wakisema Serikali haina dini. Wanasema hivyo kwa kutambua kuwa wananchi wake ndiyo wenye dini ambazo wanaenda kuabudu. Kila dini kwa namna moja au nyingine imekuwa na mchango mkubwa katika jamii. Tumeshuhudia mchango mkubwa unaotolewa na dini mbalimbali nchini kat ika kuunganisha wananchi.

 Kwa sehemu kubwa Serikali y a Ta n z a n i a ime k uwa n a uhusiano mzuri na viongozi wa dini mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wake wananufaika. Ingawa Serikali haina dini lakini ina imani kubwa na viongozi wa dini. Wanatambua msaada wake katika maeneo mbalimbali. Sote ni mashahidi jinsi marais wote waliopita akiwepo ambaye yupo madarakani kwa sasa ni waumini wazuri wa dini zao na ndiyo maana inapofikia mambo yanapokuwa magumu huhitaji msaada wa viongozi wa dini. Wanaofuatilia mfumo wa nchi yetu watabaini kuwa pamoja na kwamba katiba inasema serikali haina dini, ukweli ni kwamba hatuwezi kutenganisha serikali na dini na ndiyo maana rais hawezi kuapishwa bila kuwepo kwa viongozi wa dini. Viongozi wanaoapishwa huwa ni lazima wasome dua zao, hivyo na hicho ni kielelezo kuwa mlango mwingine serikali yetu inaamini dini. Jambo la kupongeza katika mfumo wa nchi yetu haijawahi kutokea wananchi wa Tanzania wakamchagua mtu ambaye hajawahi kuwa na dini. Karibu kila mtu mambo yake mengi yanapokwama huwa hana ujanja zaidi ya kuhitaji msaada kutoka kwa Mungu kupitia viongozi
wa dini.
Baada ya maombi wengi huwa wanaamini tatizo litaisha, hivyo karibu kila mwanadamu katika nchi yetu anaamini kuwa Mungu ndiye hatua ya mwisho ya kulilia matatizo. Mwenyekiti wa Good News For All, Askofu Chales Gadi, anasema; "Nimeandaa mkakati mkubwa wa kuigeuza Tanzania Paradiso kwa kuhakikisha maisha ya Watanzania yanakuwa kwenye Neema." Anasema, ana imani kubwa na kile ambacho amekuwa akifanya kupitia mkakati wake wa maombi sehemu mbalimbali za nchi. Anaeleza kuwa, anaamini
kwamba hali ambayo wananchi wa Tanzania wanayo siyo haki yao kuishi hivyo na watu kuw maskini.
"Na p e n d a k uwa amb i a Watanzania kuwa nchi yetu si maskini, ni tajiri na ili utajiri huu tuweze kuufaidi, kuna mambo muhimu ambayo tunahitaji kufanya kwa serikali kusikiliza ushauri kutoka kwa watumishi wa Mungu, kwani hao ndiyo wenye majibu na nchi hii," anasema."Baada ya kugundua hali
ambayo Watanzania tunaipitia si yenyewe, nimechukua hatua ya kutangaza mkakati wa kufanya maombi 14 muhimu yanayogusa taifa ambayo Mungu atajibu kwa siku 1,000," anasema na kuongeza kuwa; "Siku hizi tumeziita ni siku za mabadiliko katika Taifa l e t u . " Ta n z a n i a i n a t a k iwa kuombewa pamoja na viongozi wake pia, nyanja za uchumi, kuombea shilingi ya Tanzania izidi kupata thamani, hati ya kusafiria
iheshimike.
"Tunafanya hi v yo kwani tumekuwa tukipekuliwa sana katika mataifa mengine pale tunapojitambulisha kuwa tunatoka Tanzania wakati nchi zingine hawafanyiwi hivyo," anasema. Mambo mengine ambayo wanaendelea kufanya ni ya kuombea amani, timu ya taifa, Taifa Stars ifanikiwe kucheza Kombe la Dunia, na msongamano wa foleni uweze kumalizika jijini Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.
M a o m b i m e n g i n e n i ya kukomesha mauaj i y a albino,mapato ya kodi yaongezeke mara mbili, anasema wataiombea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili iwezeshwe kufanikiwa kukusanya kodi na kuvuka malengo mara mbili. "Tumeomba pia Tanzania iondokane na bajeti tegemezi bali ijitegemee yenyewe, pia suala la mazao mbalimbali katika taifa ikiwepo samaki wa kutosha tofauti na ilivyo sasa, ambapo wananchi wamekuwa wakivua samaki wadogo na wale wakubwa wameonekana ni maalumu kwa kuuza na si kwa kuliwa, hivyo ndani ya siku 1,000 tunategemea mabadiliko makubwa," anasema. Anasema, kinacholifanya taifa kuwa duni ni athari ya dhambi pamoja na ushirikina, kwani inashangaza kwa baadhi ya viongozi wana elimu kubwa lakini bado wanaamini vitendo vya ushirikina. Anafafanua kuwa, vitendo vya
ushirikina vinavyofanywa katika klabu za mpira kwa sehemu kubwa zimesababisha timu kushindwa,
kwani mpira ni mazoezi tu na siyo ushirikina. "Kama kweli tukitaka kucheza Kombe la Dunia, wakati mimi na timu yangu ya maombi tukiendelea kuombea timu zetu ziepukane na vitendo vya kishirikina, kwani Mungu hapendi kinachotakiwa waamini maombi yetu na atakwenda kufanya mambo makubwa," anasema. Anabaisha kuwa, ushirikina pia umechangia hata samaki kupotea kwenye mito, maziwa na baharini tatizo kubwa ikiwa ni dhambi. "Dh amb i y a u s h i r i k i n a inayofanywa baharini, kwa kutupa mifuko ya kondomu iliyotumiwa kwenye uzinzi ni mambo ya kukemewa," anasema. Anaongeza kuwa, wanaovua samaki kwa kutumia baruti waache mara moja, kwani wamekuwa wakiathiri viumbe wa baharini wakiwepo samaki. "Katika maombi haya tunaamini Mungu atakuwa ana jibu moja baada ya jingine na mpaka siku 1,000 zitakapoisha atakuwa amejibu yote ambayo tumeomba na kuanzia sasa," anasema na kuongeza;
"Watanzania wataanza kula samaki kwa wingi, kwani hilo Mungu anakwenda kulijibu haraka na uchumi wa wavuvi utapanda." Anasema, baaada ya siku hizo kukamilika Tanzania itakuwa imetimiza ile ndoto ya maisha
bora kwa kila Mtanzania kwani maombi yanakwenda kuliinua taifa.

No comments:

Post a Comment