27 February 2012

Msumbiji watamani vikao nchini virejeshwe tena

SERIKALI ya Msumbiji imeiomba
Tanzania kufikiria uamuzi wa kurejeshwa tena utaratibu wa kuwa na vikao vya pamoja kati ya pande hizo mbili ambao ulilenga zaidi kuimarisha ujirani mwema.



Ombi hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Bw.Zakaria K u p e l l a w a k a t i a k i f a n y a mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ofisini kwake mjini Vuga  visiwani Zanzibar.

Bw.Kupella alisema, Tanzania ilikuwa mstari wa mbele katika kusaidia ukombozi wa mataifa ya Bara la Afrika ikiwemo Msumbiji, hivyo ni vyema vikao vya ushirikiano vikafufuliwa kwa nia ya kulinda umoja na udugu wa sehemu hizo mbili. ''Si jambo la kupendeza kuona sasa ni mwaka wa saba pande hizo hazijakutana katika ule mfumo wa vikao vya ushirikiano. kikao cha mwisho kilifanyika mwaka 2006 nchini Msumbiji wakati kile kinachofuata kilitakiwa kifanyika Tanzania," alifafanua Balozi Kupella.Balozi wa Msumbiji alisisitiza kwamba, yapo maeneo mengi ambayo wananchi wa pande hizo mbili wamekuwa wakishirikiana pamoja hasa ikizingatiwa kwamba nchi hizo zimepakana. Alisema, itapendeza iwapo utaandaliwa utaratibu wa kuyaunganisha makundi ya vijana wa pande hizo mbili kujenga Taifa katika mpango wa kujitolea.''Ipo miradi ya jamii kama vile ujenzi wa shule na vituo vya afya, hata visima vya maji ambavyo wanaweza kutumia wanafunzi wa kujitolea wa sehemu hizo kuongeza nguvu zao," alisema Balozi Kupella.Alisisitiza kwamba ni vyema kwa nchi hizo zikafaidika pamoja katika kutumia rasilimali zilizomo kwa vile zilishirikiana katika ukombozi. Naye Makamu wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi alimueleza Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Bw.Zakaria Kupella kwamba, uhusiano wa pande hizo mbili hivi sasa inafaa uelekezwe zaidi katika uchumi badala ya siasa.

No comments:

Post a Comment