16 February 2012

Watanzania watakiwa kuwathamini watoto

Na Joseph Mwambije, Ruvuma

WANANCHI nchini hususani Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kuwathamini na kutowatelekeza watoto wenye ulemavu kwenye vituo vya kuwalea badala yake wanapaswa kuangalia namna ya kujenga ushirikiano na vituo hivyo ikiwemo kukubali kuwa wazazi wa watoto hao.

Mwito huo ulitolewa juzi na Kingozi wa Kanisa la Annoited Mission mkoani humo, Mtume Eusto Chanangula wakati akitoa msaada wa katoni za sabuni, nguo  na vifaa vya shule wenye thamani ya sh.milioni moja kwa watoto walemavu na yatima katika Kituo cha Loreto Huduma wilayani Mbinga mkoani humo.

Pamoja na kutoa msaada huo alijumuika na watoto hao kula chakula cha pamoja
cha mchana kwa lengo la kuwafariji ili wasijisikie kuwa wametengwa mbele ya jamii.
 
Naye mlezi wa kituo hicho, Bi.Augusta Mlelwa anayeshughulikia malezi ya
watoto hao alisema, changamoto waliyonayo ni wazazi wa watoto hao kuwa wakiwaleta kituoni hapo hutokomea moja kwa moja na hawaonekani tena kuwaona watoto hao.
 
Alisema, tatizo jingine linalowakabili ni baadhi ya watoto wenye ulemavu unao wezekana kuwanyosha viungo vyao katika Hospitali ya Muhimbili gharama huwa kubwa na wao wanashindwa kuzimudu. 
 
“Kituo chetu kina watoto 86 kati ya hao walemavu 56 na 30 wakiwa ni wale
wanaoishi katika mazingira magumu hivyo ni vyema jamii ikatambua kuwa kuna kazi ya kuwathamini watoto hawa,”alisema.

Kwa upande wake Bi.Rose Mahenge ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili  aliyeongozana na Mtume Channgula wakati wa kuwafariji watoto hao alisema, kuwa anatafanya mpango wa kuwashawishi waimbaji wenzake ili waangalie namna ya kuwasaidia watoto hao wenye ulemavu kwa kuwapa misaada mbalimbali inayohitajika

No comments:

Post a Comment