15 February 2012

Wataka nchi za EAC kuongeza bajeti mapambano ya rushwa

Na James Gashumba, EANA

WAJUMBE wa mkutano wa kamati ya Sekta ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (ECA) wametoa changamoto kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kutenga fedha kwenye bajeti zao za kitaifa kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za
mapambano dhidi ya rushwa.

Wajumbe hao walieleza kwenye maazimio yao mwishoni mwa kikao chao Arusha, Tanzania kwamba bajeti inayotolewa na EAC ni ndogo kuweza kukidhi haja ya watendaji waliomo kwenye vita dhidi ya rushwa.

Shirika la Huru la Habarai la Afrika Mashariki (EANA) limeripoti kwamba katika maazimio hayo pia walizishauri nchi wanachama kutumia teknohama wakati wa kuwahoji washukiwa wa uhalifu wa rushwa kama mbinu moja ya kuimarisha taratibu za ulinzi wa ushahidi.

Mapema wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu wa EAC, anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Beatrice Kiraso, alirejea mwito wake kwamba kanda hiyo ya ECA, imedhamiria  kuongeza juhudi katika mapambano
dhidi rushwa na kuzingatia maadili na utu katika suala zima la mtangamano wa katika kanda.

"Nahitaji kusisitiza kwamba jambo hili ndiyo nguzo kuu ya itifaki ya utawala bora na ni utekelezaji wa msingi muhimu wa Jumuiya," alisema.

Kwa mujibu wa Kiraso mswada huo unatarajiwa kutiwa saini katika kikao maalum cha wakuu wa EAC  kitakachofanyika hivi karibuni.

Kakao cha kamati ya Sekta ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa EAC kiliitishwa kwa lengo la kupata maendeleo ya hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa wa
makubaliano yaliyofikiwa katika vikao vilivyotangulia vya Baraza la Mawaziri.



1 comment:

  1. Katika hili suala la kupambana na Rushwa, Tanzania na nchi nyingine zijifunze kutoka Rwanda kuanzia mfumo wa serikali ya Rwanda ya ZERO CASH, (yaani ofisi za Serikali haziruhusiwi kushika au kulipa fedha taslim kazi yao ni kuhusika na makaratasi tu), uthbiti wa Manunuzi ya Umma,Ufuatiliaji wa karibu wa sheria, utoaji haki mahakamani na kutoa adhabu zinazozuia wengine kuiba au kufuja mali za wananchi. Nchi ya Rwanda ni ndogo lakini inayo mengi sana ya kuigwa.

    Nchi nyingine zisione aibu kujifunza kutoka kwao. Hakuna haja ya kwenda Ulaya au kufanya makongamano ambayo hayana tija. Rushwa imekuwa wimbo. Huwezi kuondoa rushwa kabisa lakini inawezekana kuipunguza kwa kiasi KIKUBWA. Rwanda imefanikiwa kwa hilo na bado inaendelea na jitihada za kutokomeza Rushwa.

    Tanzania iache mambo ya Kuunda Tume kujadili wezi. Polisi wapo, mahakama zipo. Katiba ipo. Taasisi husika ziachwe zifanye kazi zao. Hizi tume zitumike kwenye masuala ya kisiasa na kuchunguza kama vyombo vinavyohusika kupambana na vinatenda haki. Ina maana serikali au vyama vyetu havina imani na Mhimili wao wa Mahakama au Polisi au taasisisi zilizoundwa na Bunge?

    Polisi waachiwe wanyonge na vyombo vilivyoundwa kama TAKUKURU viachiwe vishughulike wakubwa pale wanapoiba au kupokea au kutoa rushwa ili wapate VIP treatment?
    Wizi au ulaji rushwa hauna tabaka.

    ReplyDelete