Na Rehema Mohamed
WIZARA ya Mambo ya Nje ya na Ushirikiano wa Kimataifa, inakabiliwa na ufinyu wa bajeti kutokana ile inayotolewa na Serikali kuwa haikidhi uendeshaji wa wizara hiyo.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bw. John Haule, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alikuwa akitolea ufafanuzi kuwa taarifa zilizoeleza kuwa wizara hiyo iko hoi kifedha kiasi cha kushindwa kuwalipa mishahara mabalozi na kukosa fedha za matumizi yake ya kawaida.
Bw.Haule alisema kuwa fedha zinazokosekana ni zile za matumizi ya wizarani kama kulipa bili ya umeme, kununua mafuta ya magari, matengenezo ya magari,vifaa vya ofisi na nyinginezo.
Alikiri kuwa kuwa fedha wanazopewa hazitoshelezi na kuwa pamoja na fungu hilo kuwa dogo, lakini kipaumbele chao cha kwanza ni mahitaji ya mishahara na posho za wafanyakazi na mabalozi.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa katika kikao chake na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kilikuwa kikijadili taarifa ya Hesabu za Wizara kwa mwaka wa fedha 2009/2010 na kilichozungumziwa katika kikao hicho ni kuwa Balozi zetu bado zinatumia viwango vya
posho ya utumishi wa nje ambavyo vimepitwa na wakati.
No comments:
Post a Comment