16 February 2012

Wajiunga CHADEMA kufukuzia udiwani

Na Bryceson Mathias, Morogoro                                                  

BAADHI ya watu wameanza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Mtibwa, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro,  ili kufukuzia nafasi ya udiwani iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo,marehemu Tusekile Mwakyoma.

Kasi ya kujiunga na CHADEMA ilianza kujitokeza hivi karibuni, baada ya chama hicho kutangaza sifa za mtu
anayetaka ateuliwe kugombea nafasi hiyo

Habari zilizilifikia gazeti hili mkoani hapa, zinadai kuwa  baada ya CHADEMA kumaliza msiba, iliweka wazi  sifa za mtu atakayeteuliwa na chama hicho ili kugombea nafasi  hiyo .

“Tumebaini kasi kubwa ya waliokuwa si wananchama wa CHADEMA,  imeongozeka kwa kasi, baada ya
chama kutangaza sifa za mtu anayefaa kuteuliwa na kugombea udiwani, lakini wengi hawana lengo la kuwatumikia wananchi ila cheo ,” alisema mzee aliyekataa jina lake lisitajwe gazetini.

Majina manane ya waliotajwa kuchukua fomu za chama hicho ni  Bw. Peter Chengula, Bw. Pangrasi Kahinga, Bw. Lukasi Mwakambaya, Bw. Nassoro Manyama, Bw. Joshua Mshigati, Bw. Weliimo Lyimo, Bw. Mrisho Mohamed, na
Christian Seif.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya Bw. Yusufu Mtamatale Mbaga alipoulizwa kwamba inadaiwa katika kundi hilo
kuna mamluki waliojiunga kwenye chama ili kuwavurugia uchaguzi

Marehemu Bi. Mwakyoma (28) alifariki Januari mosi, mwaka huu, baada ya kuchomwa kisu chini ya titi.


No comments:

Post a Comment