Na Rachel Balama
TANZANIA ni miongoni mwa nchi 37 zilizoridhia kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership - OGP) ikiwa ni juhudi za kimataifa za kuhimiza uendeshaji wa Serikali kwa uwazi zaidi.
Hatua hiyo inalenga ushirikishaji wa wananchi, kudhibiti rushwa ndani jamii na kuimarisha utoaji wa huduma bora.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaama jana na Ofisi ya Rais kupitia tamko la Serikali, mpango huo uliozinduliwa na viongozi wa nchi mbalimbali wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mjini New York, Marekani.
"Kwa kutambua umuhimu wa Mpango huu, Tanzania imeridhia kujiunga nao," ilieleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa Tanzania ni nchi ya 37 kuridhia kujiunga na mpango huo zikiwemo nchi nne za Afrika, ambazo ni Afrika ya Kusini, Ghana, Kenya na Liberia", alieleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa vigezo vya nchi kuwa mwanachama wa Mpango huu ni pamoja na kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na wananchi.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Serikali imeanza mchakato wa kutayarisha Mpango Kazi wa Kitaifa katika kuandaa mpango huo na wananchi watashirikishwa kikamilifu ili kutoa maoni yao kuhusu maeneo yatakayozingatiwa.
No comments:
Post a Comment