Na Salim Nyomolelo, Utete
MAKAMU wa Rais Dkt.Gharib Mohammed Bilal amewahakikishia wananchi wa Utete, Wilaya ya Rufuji mkoani Pwani kuwa serikali itahakikisha inaboreshea huduma ya umeme ili upatikane kwa uhakika.
Dkt.Bilal aliyasema hayo juzi katika hotuba yake baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.
Aliwaambia wananchi wa Utete kuwa atahakikisha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasambaza nguzo za kutosha ili kuwarahisishia wananchi kuunganisha umeme kwa gharama nafuu.
Katika ziara hiyo, Dkt.Bilal alizindua jiwe la msingi la nyumba 14 za watumishi, jengo la ofisi ya CCM na baada ya hapo alikwenda kuzungumza wa wanachama wa CCM.
"Kwa sasa huduma ya umeme ipo, lakini bado kuna idadi kubwa ya kaya ambazo hazinufaiki na huduma ya nishati, hii, hivyo ninawahakikishieni kuwa TANESCO watasambaza nguzo ili muweze kuunganisha umeme kwa gharama nafuu," alisema Dkt.Bilal
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufuji, Bw.Seif Rashid, alisema endapo ahadi hiyo itatekelezwa utakuwa ndani ya mwaka mmoja wananchi wa Utete wataunganishiwa umeme kwa gharama za sh.75,000.
Alisema waliamua kuomba shirika hilo kutokana wananchi wa eneo hilo kutokuwa na kipato cha kutosha cha kuwajengea uwezo wa kunufaika na nishati ya umeme.
"Wananchi wengi wa hapa utete wanashindwa kumudu gharama za kuunganisha umeme kwa sababu hakuna nguzo jirani,kwa hiyo mradi huu utasaidia kuunganisha umeme kwa gharama ya sh.75,000 kwa kila kaya," alisema Bw.Rashid.
No comments:
Post a Comment