16 February 2012

Tanroads mko wapi?



                           Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli


Mhariri Majira

NAOMBA nafasi katika gazeti lako niweze kutoa kero iliyodumu kwa muda mrefu katika barabara ya Kigogo.

Kuanzia  roundabout ya Kigogo hadi kituo cha randa bar ni sehemu ya kona ambayo imepoteza maisha ya watu wengi na kuendelea kwa ajali hizo bila wahusika kuweka matuta.

Mkandarasi aliyekuwa anajenga alikuta kuna matuta na alama za kivuko cha waenda kwa miguu, lakini baada  ya kumaliza ujenzi hakuweka alama hizo.

Matokeo yake wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Kigogo wanagongwa kila siku pamoja na wananchi wanaotumia barabara hiiwanapoteza maisha na wengine kupata vilema vya maisha huku jitihada za kuokoa maisha hazionekani.

Tumechoka kushuhudia vifo vinavyotokana na hizi ajali, tuanataka matuta na alama zote ili kupunguza kuwapoteza wanafunzi amabo ni taifa la kesho.

Natoa wito kwa wakandarasi wanaojenga barabara kuhakikisha wanaweka vivuko ya waenda kwa miguu na kuacha kutoa sababu zisizo na msingi.

Ni kwanini tukae kwa mashaka wakati hili ni wajibu wa makandarasi. Tanroads ingilieni kati tatizo hili.

J.Zebedayo

Dar es Salaa

No comments:

Post a Comment