24 February 2012

Taifa Stars, Congo 'ngoma droo

Na Elizabeth Mayemba
Taifa Stars, jana ililazimishwa suluhu na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu hizo zinajiandaa na mechi za awali za mchujo wa kuwania kufuzu michuano ya Afrika, itakayofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Mechi hiyo ilianza kwa nguvu, ambapo dakika ya tatu Congo ilikosa bao kupitia kwa Angani Kayiba, baada ya kupata nafasi nzuri ya kufunga lakini akashindwa kuitumia.

Stars nayo ilijibu shambulizi hilo dakika ya sita kupitia kwa Hussein Javu, ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa Shedrack Nsajigwa hata hivyo akapiga 'shuti mtoto'.

Dakika ya 15 John Bocco wa Stars alishindwa kuifungia bao timu yake baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mwinyi Kazimoto, hata hivyo shuti lake lilidakwa na kipa Konga Borongo wa Congo.

Bocco alikosa tena bao lingine dakika 45, baada kuambaa na mpira kuanzia katikati ya uwanja na kuachia shuti kali, lililopaa nje ya mwamba.

Kipindi cha pili Stars iliwatoa Juma Kaseja, Mrisho Ngassa, Hussein Javu na Abdi Kassim 'Babi' na kuwaingiza Mwadini Ali, Nsa Job, Uhuru Selemani huku na Salum Abubakari 'Sure Boy'

Congo nayo iliwatoa kipa Borongo na Tresor Mputu na nafasi zao kuchukuliwa na Kidiaba Muteba na Emomo Ngoy.

Mabadiliko hayo yaliongeza upinzani kwa timu zote ambapo dakika ya 51, Ilunga wa Congo alikosa bao baada ya mabeki wa Stars kufanya uzembe wa kujichanganya lakini shuti lake likapita pembeni ya mwamba.

Dakika ya 61, Stars nayo ilikosa bao kupitia kwa Bocco ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa Babi.




No comments:

Post a Comment