JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke limeweka mikakati ya kuwasaka wananchi wanaofanya vitendo vya uhalifu ikiwa pamoja na biashara ya shaba.
Akizungumza na Majira Dar es salaam jana Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Bw. David Misime alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakikimbilia wilayani Temeke kufanya uhalifu kwa madai kuwa hiko ndiko kwenye viwanda vingi pamoja na bandari.
Kamanda alisema kuwa Jeshi lake limejipanga kikamilifu kwa ajili ya kupambana na wahalifu hao ambao wamegeuza Temeke ndiyo sehemu ya kufanyia biashara hiyo.
Alisema hivi karibuni wamebaini kuwepo kwa wahalifu ambao wanafanya biashara ya vyuma aina ya shaba na kukimbilia wilayani humo kwa ajili ya kufanya biashara hiyo, Jeshi limejipanga ili kuhakikisha wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Wakati huo huo Kamanda Misime alisema Jeshi hilo limewakamata watuhumiwa 125 wa matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo ya unyang'anyi wa kutumia silaha, kukaba pamoja na kuuza madawa ya kulevya.
Alisema kuwa watuhumiwa 25 wakutumia silaha nzito za kwenye majumba, 55 watuhumiwa wa kuuza madawa yakulevya 11, watuhumiwa wa kuuza bangi na gramu 15 za madawa ya kulevya na wengine 21 walikamatwa na lita 24 za pombe haramu ya gongo.
Alisema kuwa katika operesheni hiyo walifanikiwa kuwakamata wapiga debe na wacheza kamali 20,madereva 177 wa magari na wa pikipiki 13 kwa makosa ya usalama barabarani na wote wamefikishwa Mahakamani na wengine SUMATRA.
No comments:
Post a Comment