Baraza la Habari Tanzania (MCT) limewaapisha Majaji 11 kwa ajili ya kusaidia kuwapata washindi wa tuzo bora za waandishi wa habari (EJAT)
Akizumgumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya baraza hilo, Jaji mstaafu, Bw.Thomas Mihayo alisema taaluma ya uandishi wa habari inapitia katika kipindi cha mpito ambacho ni kutoka waandishi legelege hadi kuaminika nasiyo nchini tu bali hata duniani kwa ujumla.
"Kazi ya ujaji ni ngumu na waombaji ni wengi wote wamefanya kazi nzuri hivyo ni kazi inayohitaji umakini ili kupata washindi na naamini matokeo yakitoka basi hakutakuwa na malalamiko yoyote kutoka kwa washindani," alisema
Alisema kuwa kuapa ni desturi iliyoanza tangu enzi za mababu na kuapishwa sio kwamba hawahaminiki bali mnaaminika lakini kuapa pia ni taratibu zilizo wazi.
Naye Katibu wa baraza hilo, Bw.Kajubi Mkajanga alisema tunawaapisha majaji watakaosaidia kuwapata washindi wa tuzo za waandishi bora wa habari.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo ya majaji, Bw.Wense Mushi alisema hali hii inaonesha ni jinsi gani baraza la habari linavyokubalika baada ya kutangaza mashindano hayo wamepata kazi nyingi sana kutoka kwa wanahabari kupitia redio,tv na magazeti
"Nalishukuru baraza la habari nchini kwa kutuamini na kutuchagua sisi kuwa majaji wa tuzo hizo na tunawaahidi kufanyakazi kwa umakini sana kwa kuwa MCT inaaminika na wanahabari
Katika hafla hiyo walioapishwa kuwa majaji wa EJAT kwa mwaka huu ni Bw.Wense Mushi ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo,Bw.Yusuph Chunda,Bw.Mwanzo Milinga,Bi.Eda Sanga,Bi. Prudensiana Temba,Bw.Anaklet Rwegayula na Bi.Pili Mtambalike.
No comments:
Post a Comment