06 February 2012

Aparamia ukuta na kufa

MTU mmoja asiyefamika jina lake amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akiendesha kumshinda nguvu na kuparamia ukuta.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Kipolisi Mkoa wa Kinondoni, Bw.Charles Kenyela alisema jana kuwa marehemu ambaye alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 608 AMR alipatwa na umahuti huo usiku wa kuamkia jana baada ya gari hilo kumshinda wakati alipokuwa akitokea Mikocheni B barabara ya Bagamoyo.

Kamanda Kenyela alisema kuwa dereva huyo anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 au 30 alikuwa akitokea Ostarbay kuelekea Kawe aligonga ukuta wa nyumba Block namba 107 na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

Alisema kuwa marehemu alipatwa na umauti huo wakati alipokuwa akiendesha gari kwa mwendo kasi na kwamba gari hilo limehifadhiwa katika Kituo KIkuu cha Polisi Ostarbay na jeshi linaendelea na upelelezi.

Wakati huohuo jeshi la Kipolisi Mkoa wa Temeke linaendelea na upelezi wa kuungua Kiwanda cha magodoro cha Pan Afrika kilichopo barabara Mbozi Changombe.

Kwa mujibu wa Kamanda Kipolisi David Masime alisema kuwa moto huo uliunguza kiwanda hicho majira asubuhi jana na kuteketeza mashine za umeme na chanzo chake kinadaiwa itilafu ya umeme.

No comments:

Post a Comment