23 February 2012

Hukumu ya wavuvi samaki wa magufuli kutolewa leo

Na Rehema Mohamed

HUKUMU Kesi ya Uvuvi haramu wa samaki katika Ukanda wa Kiuchimi wa Tanzania, inayowakabili raia watano wa kigeni inatarajiwa kutolewa leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo maarufu kama kesi ya Samaki wa Magufuli, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kufanya shughuli za uvuvi katika Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania (EEZ), bila kuwa na kibali na kuchafua mazingira ya bahari.

Washtakiwa hao ni pamoja na Bw.Hsu Chin Tai ambaye ni Naodha wa meli waliyokuwa wakiitumia kwa shughuli za uvuvi Tawaliq 1 .

Wengine ni Bw.Zhao Hanquing na  Bw.Hsu Sheng Pao ambao wote ni mawakala wa meli hiyo, pamoja na wahandisi  wawili wa meli hiyo, Bw.Cai Dong Li na Bw.Chen Rui Hai.

Washtakiwa hao wanatetewa na wakili Bw.Ibrahimu Bendera na Bw.John Mapinduzi, huku upende wa Serikali ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Bw.Muganga Biswalo akisaidiana na Mawakili wa Serikali Bw.Prosper Mwangamila na Bw.Peter Maugo,

Kesi hiyo ipo mbele ya jaji Agustine Mwarija. Machi 9 mwaka 2009 washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa kosa hilo.

Washtakiwa hao walikamatwa katika operesheni ya kulinda rasilimali za Tanzania iliyokuwa ikiendeshwa na Serikali wakati Dkt. Magufuli akiwa ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi.


No comments:

Post a Comment