25 January 2012

'Wafanyabiashara Mbeya acheni kuibia serikali'

Na Esther Macha, Mbeya

WAFANYABIASHARA  wa Mbeya wameshauriwa  kuacha kuibia serikali mapato baada ya kupangishwa na halmshauri na wao kupangisha watu wengine bila kulipa ushuru .


Halmashauri hiyo imetoa onyo kali na kusema  kuwa yeyote atakae bainika kufafanya hivyo ataondolewa ili vyumba hivyo wapewe watu wengine ambao ni waaminifu na
ambao wako tayari kufanya biashara pamoja na kulipa ushuru kama inavyotakiwa.

Hayo yalisemwa  mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bw.Juma Iddi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Bw.Iddi alisema wamegundua mchezo mchafu unaofanywa na wafanyabiashara hao wanapopangishiwa vyumba na Halmashauri ya jiji kwa bei ndogo lakini wao hupangisha kwa wengine kwa gharama kubwa zaidi kitendo ambacho si cha kizalendo.

Alisema kitendo hicho ni kuiibia mapato serikali hivyo kwa yeyote atakaye bainika anafanya hivyo ataondolewa ili vyumba hivyo wapewe watu wengine ambao ni waaminifu na ambao wako tayari kufanya biashara pamoja na kulipa ushuru kama inavyotakiwa.

Alisema Serikali imekuwa ikiwapangisha kwa gharama ya shilingi 50,000 kwa chumba kimoja lakini wao hupangisha kwa watu  wengine kwa zaidi ya shilingi 500,000 ambapo yule mtu ananufaika na kulipia gharama ndogo halmashauri huku yeye akivuna fedha nyingi.

“Natoa onyo kwa mfanyabiashara yeyote atakayebainika kufanya wizi huo tutamuondoa halafu tutamfikisha kwenye vyombo vya sheria kwa kuhujumu uchumi maana kama sisi tulimpangisha chumba kwa shilingi 50,000 iweje yeye apangishe kwa gharama kubwa,” alisisitiza Mkurugenzi.

Aliongeza kuwa wapo katika mpango wa kuandaa mikataba mipya ambayo watabaini wote ambao hawatakuwa wafanyabiashara na wanachukua vyumba ili wapate udalali kwa kuwapangisha watu wengine watawafukuza mapema ili kuongeza mapato kwa serikali.

No comments:

Post a Comment