25 January 2012
Uchumi kwa waathirika wa vipodozi kushuka
Na Esther Macha,
Mbeya
MKURUGENZI Mkuu Mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA )Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Bw.Paul Sonda amesema mbali na athari za matumizi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kuna hatari ya uchumi kushuka kwa waathirika kutokana na gharama kubwa za matibabu
na wengine kupoteza maisha.
Alisema kuwa pia kuna hatari wengine kupata ulemavu wa maisha kwani hatua hiyo imekuja baada ya utafiti kuonesha bado baadhi ya wafanyabiashara wanavipitisha kwa njia ya panya.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi huyo katika Mkutano Mkuu wa Madaktari wa Hospitali na Zahanati binafsi uliofanyika jiji hapa.
Bw.Sonda alisema kuwa watu wanaotumia vipodozi hivyo wanahatari kubwa ya kukumbwa na magonjwa ya kupoteza fahamu, kansa ya damu, kansa ya ini, ubongo, pia kwa akina mama wajawazito kujifungua watoto wenye
mtindio wa ubongo, muwasho mwilini na kunenepa kupita kiasi.
Hata hivyo Bw.Sonda amesikitishwa na kitendo cha wakazi wa Songwe ambapo vipodozi hivyo viliteketezwa baada ya kuchukua masalia ya vipodozi hivyo na kuvitumia.
Hivi karibuni Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini waliteketeza vipodozi vyenye thamani ya sh.mil.129.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment