25 January 2012

Na Rachel Balama

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyarandu amesema kuwa nchi haiongozwi kwa wizi, ufisadi bali inaongozwa kwa kufanyakazi kwa bidii na ataendelea kuchapa kazi si kwa kutafuta urais bali kwa kujitolea ili kumsaidia rais na kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Ataka makundi yanayorumbana  na kuchafuana ndani ya CCM  kwa kutafuta urais wa mwaka 2012 kusubiri kwa kuwa muda wa kufanya hivyo bado haijafika na kuwataka wafanye kazi.

Ameyataadharisha makundi hayo kwamba yeye hana nia na wala hataki kugombea urais hivyo hakuna haja ya Tanzania kuwa na makundi ya kisiasa kwa lengo la kutafuta urais.

"Sifanyikazi kwa kutafuta sifa ya kuwa mgombea urais mwaka 2015 ila nafanyakazi kwa kuwa rais aliniteua ili nimsaidie katika baadhi ya majukumu na nitafanya hivyo ili kutekeleza ilani ya CCM.

"NIlipewa nafasi ya unaibu waziri na rais si kwa ajili kwamba hapo baadaye nije kuwa rais hapana nafanyakazi ili kutekeleza ilani ya chama changu kwa kujua kwamba nawatumikia watanzania wenzangu.

Alisema hawezi kukaa bila kuzungumza na mtu yoyote hapa nchini eti kwa kuonekana kwamba yupo kundi fulani, wenye nia ya urais wasubiri.

Bw. Nyarandu alikanusha habari kwamba anafadhiliwa na marekani ili awe rais na kuongeza kwamba wanaomzushia wana lengo la kumchafulia jina kwa kuwa wanadhani kwamba yeye ni miongoni mwa wagombea urais..

Ataka watanzania wote bila kujali itikadi kufanyakazi kwa bidii, ubunifu ili kuwa sehemu ya nchi inayopiga hatua kimaendeleo.

Awataka wanasiasa wa CCM kutekeleza ilani ya chama chao kwa vitendo na kusimamia utekelezaji wa ilani hiyo na kuachana na siasa za makundi kwa kutojengeana chuki.

Kuhusu umeme

Alisema kuwa athari za kupanda kwa bei ya umeme hakuwezi kuwafanya wawekezaji kuondoka kama ambavyo nchi isingekuwa na umeme kabisa hata hivyo umeme umepanda kwa muda.

ALisema kuwa umeme umepanda kutokana na tatizo la upatikanaji wa umeme ni kubwa lakini serikali inajitahidi kuwekeza vya kutosha kuzalisha umeme kwa wenye viwanda na majumbani.

Alisema kuwa japo bei imepanda lakini serikali inajitahidi kuhakikisha umeme unapatikana muda wote na tayari Tanzania itakuwa ni nchi inayozalisha umeme wa makaa  ya mawe.

Ubinafsishaji

Alisema kuwa kuna baadhi ya viwanda mfano wa kiwanda cha korosho ambacho kimekufa, serikali inaangalia mikataba mipya na kama kuna ulazima wa viwanda hivyo vitarudishwa kwa uuma.

Kwa upande wa vile vilivyobadilisha matumizi sio tatizo ili mradi waongeze mitaji yao.

Kuhusu kiwanda cha General Tyre kilichopo Arusha, alisema kiwanda hicho kilikuwa ni muhimili mkubwa wa viwanda mkoani Arusha na serikali imesikika kwa kiwanda hicho kufungwa.

Hata hivyo kwa kutambua umuhimu wa kiwanda hicho kitafunguliwa na kitamilikiwa na SHirika la MAendeleo la Tifa(NDC) ambapo pia atatafutwa mbia atakayefanya kazi na shirika hilo.

Alisema kiwanda hivho kitaanza kazi mara baada ya taratibu zote kukamilika.

ALisema shirika la NDC lina uwezo wa kutekeleza majukumu yote na tayari limeashaanza mradi wa kuchimba na kuyeyusha chuma cha pua katika eneo la linganga na limekwisha saini dola bilioni  tatu.

ALisema katika mradi hyo yale mabaki ya makaa ya mawe yuatatumiaka kutengeneza umeme wa megawati 600 ambapo alisema kuwa katika mradi huo hakutakuwa na ufisadi wa aina yoyote

Kuhusu bidhaa feki

Alisema kuanzia Januari mwaka huu serikali imeamua kukagua bidhaa kabla hazijaingia nchini kupitia shirika la viwango nchini tbs.

Alisema ni vyema wazalishaji wa bidhaa zozote nchini ni lazima wapate vibari kutoka TBS ikiwani ni pamoja na matuta ya barabarani ambayo ni lazima yawe na  viwango

Ajira

Alisema kuwa katika viwanda vingi hapa nchini wazalishaji wake ni vibarua amabo hawana mikataba ya kudumu lakini serikali imeliona hilo na sheria za kazi zipo wazi.

Aliwataka watanzania kupewa fursa kwa kazi ambazo wanaziweza na utofauti uwepo kwenye zile kazi zenye utaalamu wa kutosha.

No comments:

Post a Comment