Na Makumba Mwemezi
Mwaka 2012 huwenda ukawa mgumu zaidi kwa watanzania hasa wenye kipato cha chini, kutokana na Serikali kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei ambao umepelekea benki za biashara kupandisha viwango vya riba za mikopo kutoka wastani wa asilimia 23 Mwishoni mwa mwaka jana hadi wastani wa asilimia 45 kuanzia Januari Mwaka huu.
Taarifa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa zinaonesha kuwa Mfumuko wa Bei umezidi kuongezeka kutoka chini ya asilimia 5 mwanzoni mwa mwaka jana hadi asilimia 19.2 mwishoni mwa Mwezi Novemba 2011, na kuathiri kwa kiasi kikubwa uwezo wa shilingi katika kufanya manunuzi.
Kupanda kwa viwango vya riba za mikopo katika mabenki ya biashara si tu kuwa kutaathiri mwenendo wa urejeshaji mikopo iliyokwisha chukuliwa bali kutapunguza pia kasi ya ukopaji mpya hivyo kuathiri biashara za kibenki na uwekezaji.
Akizungumza na Majira katika mahojiano maalumu, Mwenyekiti wa Chama cha wenye Mabenki Tanzania na ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru amethibitisha kupanda huko kwa viwango vya riba za mikopo ya benki na kuutaja mfumuko wa bei kuwa chanzo kikubwa.
Kwa Mujibu wa Mafuru sababu nyingine ambazo zimechangia ongezeko hilo ni pamoja na hatua ya serikali ya kuondoa kiasi cha zaidi ya bilioni 100 katika mzunguko wa fedha kama njia ya kudhibiti mfumuko huo, hatua ambayo imezipunguzia benki uwezo wa kukopesha kwa kukosa fedha za kutosha.
Serikali pia imeongeza viwango vyake vya amana (Deposit) zisizotozwa riba kutoka asilimia 20 mpaka 30 jambo ambalo pia linafanya kiasi kikubwa cha pesa kutokuwa katika mzunguko wa kawaida hivyo kuzikosha benki uwezo wa kukopesha na kuzalisha faida.
Aidha Mafuru alisema viwango vya kukopeshana miongoni mwa mabenki pia vimepanda kutoka wastani wa asilimia 5 mwanzoni mwa mwaka jana mpaka wastani wa asilimia 30 Mwaka huu jambo ambalo linalazimisha pia viwango vya riba za mikopo kwa wateja wao ziongezeke.
"Unaweza kuangali jinsi ambavyo mfumuko wa bei na hatua zinazochukuliwa na serikali kuudhibiti vilivyochangia kuongeza ghalama za uendeshaji wa benki, lakini pia benki zinapata pesa kwa riba ya juu kutoka vyanzo vyake, unadhani hataungelikuwa wewe unaendesha biashara hii ungechukua hatua gani" anasema Mafuru.
Hatahivyo baadhi ya wataalamu na wachambuzi wa mambo ya uchumi wamesema kama serikali na benki wakiacha viwango hivi viendelee bila kuchukua hatua ya kuvidhibiti, kutakuwa na athari hasi katika uchumi wa taifa ikiwamo kushuka kwa ukopaji na urejeshaji wa mikopo.
Bw. Adrian Njau ambaye ni mchumi katika Baraza la Biashara la Afrika Mashariki, anasema athari za muda mrefu za kushuka kwa urejeshaji mikopo na ukopaji ni benki kutopata faida, kupungua kwa uwekezaji na ufanyaji biashara, kupungua kwa ajira pamoja na kuzorotesha hali ya ukuaji wa uchumi.
"Unaweza kufikilia matokeo ya watu kushindwa kufanya biashara na kuwekeza, watu kukosa ajira na kuporomoka kwa uchumi, hapo ndipo unaweza kugundua kuwa Mwaka 2012 unaweza kuwa wa taabu kwa watanzania wengi kama serikali isipochukua juhudi za makusudi kudhibiti hali hii inayoendelea" anasema Bw. Njau.
Bw. Njau anasema jukumu kubwa ililonalo serikali katika mwaka huu ni kudhibiti mfumuko wa bei, kwa vile kama utaendelea kupanda vipato vya watabnzania waliowengi vitazidi kupungua na watu watazidi kuondoa fedha zao katika mabenki na mzunguko hivyo kuua kabisa uchumi.
Lakini baadhi ya wananchi na wachambuzi wa mambo ya uchumi wanaamini kuwa hatua ya mabenki kupandisha riba za mikopo haitokani na mfumuko wa bei, bali ni ujanja wa kujiongezea faida na kukwepa wajibu wao wa ufuatiliaji urejeshaji wa mikopo.
Msahuri wa maswala ya biashara Bw. Theodory Kaijanante anasema benki zimesahau wajibu wao wa kuhakikisha wanakopesha na kufuatilia uwekezaji wa mikopo hiyo pamoja na urejeshaji jambo ambalo limesababisha wakopaji wengi kukimbia au kushindwa kurejesha mikopo hiyo.
Alisema baada ya kuona hali hiyo benki zimeamua kuongeza viwango vya riba ili kufidia baadhi ya fedha ambazo hazikurejeswa na baadhi ya wakopaji.
"Pamoja na mambo yote wanayotaja kuwa ndio sababu ya upandishwaji wa viwango vya riba, bado benki zinawza kuwa na mchango katika kupunguza viwango hivyo kama zitajikita katika kuwasimamia wakopaji ili waweze kuzalisha na kurejesha mikopo yao kwa wakati na kwa mujibu wa makubalianoa" anadai Kaijanante.
Wadau hawa wanatoa wito kwa serikali kufikili njia sahihi za kudhibiti mfumuko wa bei na kupanda kwa ghalama za maisha badala ya kuondoa fedha katika mzunguko njia mabayo Bw. Mafuru haridhishwi nayo.
Bw. Mafuru anasema tafsiri sahihi ya mfumuko wa bei ni kuwa fedha ni nyingi katika soko kuliko bidhaa za kununua, na njia pekee ya kudhibiti hali hii sio kuondoa fedha katika mzunguko bali kuongeza uzalishaji ili pesa ipate matumizi.
"Serikali inapaswa kufikilia jinsi ya kukuza uzalishaji na kuimarisha uchumi, hivi ndivyo vitaimarisha mfumuko wa bei badala ya kujikita katika mfumuko wa bei ambao matokeo yake ni kuporomosha uchumi kwa ujumla" anasema Bw. Mafuru.
SERIKALI KUPITIA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) INALOJUKUMU KUBWA LA KUHAKIKISHA MFUMUKO WA BEI ANGALAU UNADHIBITIWA KWA KIASI. MOJAWAPO YA MBINU ZA KUDHIBITI MFUMUKO HUU NI KUCHUNGA MATUMIZI NA MAPATO YA FEDHA ZA KIGENI.
ReplyDeleteGAVANA WA BENKI ANA JUKUMU LA KUHAKIKISHA KUWA AKIBA YETU YA FEDHA ZA KIGENI INASIMAMIWA, INABORESHWA NA KULINDWA VIZURI ILI IONGEZEKE NA KUIWEZESHA NCHI KUAGIZA MALI NA BIDHAA MUHIMU.
WATANZANIA TUMUULIZE GAVANA WETU MASWALI YAFUATAYO;
1. FEDHA ZA KIGENI ZINAZOTOKANA NA MAUZO KAMA YA MADINI HUSUSAN DHAHABU, ALMASI, TANZANITE, N.K NA ZA MAZAO MENGINE YA BIASHARA ZINAINGIZWA KWENYE AKAUNTI YA BENKI YETU KWA KIASI KINACHOTAKIWA/ BEI TUNAZOLIPWA NI SAHIHI AU ZINAKUWA UNDER DECLARED? BENKI INAHAKIKISHA MAZAO KAMA KAHAWA, PAMBA CHAI NK. IKIUZWA NJE NA WAFANYA BIASHARA BINAFSI FEDHA ZOTE ZINAWASILISHWA KWA USAHIHI? FEDHA ZA MADINI ZINAZOINGIA KILA SIKU KWA MAMILIONI INDIA STREET DAR NA MADINI KUUZWA NJE, FOREX ZAKE ZINAINGIA NCHINI? KIPINDI CHA COOPERATIVE NA MASHIRIKA YA UMMA ANGALAU ZILIKUWA ZINAFUATILIWA NA ZINAWASILISHWA KWA SAHIHI.
2. HIZI FEDHA KIDOGO ZA NJE ZINAZOKUSANYWA NA BUREAU DE CHANGE KUTOKA KWA WATALII NA WATU WENGINE WA DIASPORA KWA NIABA YA BENKI KUU ZINAFIKISHWA BENKI KUU KWA KIASI KAMA INAVYOTAKIWA?
INAONAONEKANA WAZI WAZI KUWA KUNA WATU WANAOCHOTA FEDHA HIZI ZILIZOKUSANYWA NA HIZI BUREAU NA KUZITUMIA KWA MANUNUZI AU PENGINE MATANUZI NJE YA NCHI BILA KUIDHINISHWA NA BENKI.
3. FEDHA ZA KIGENI ZINAZOTUMIKA KULIPA KARO ZA WANAFUNZI NJE YA NCHI ZINATOKA WAPI? ZA BIASHARA ZA DUBAI, CHINA, MAGARI YA JAPAN ZINATOKA WAPI? INA MAANA FEDHA ZOTE HIZO WAHUSIKA NA BIASHARA HIZI WANAFANYA KAZI AU BIASHARA NCHI ZA NJE WANAKOZIPATA?
SISI WATANZANIA HATUWEZI KUACHIA FEDHA ZETU ZIENDE NJE KIHOLELA. HATA MERIKANI WENYE DOLA WANAZUIA KWA WAKATI MWINGINE!
KAMA MTANZANIA, NAMSHAURI GAVANA WETU "AMANAGE" VIZURI FEDHA NA SIO WATU. BILA KUFANYA HIVYO TAIFA LITAANGAMIA KIUCHUMI. AJIFUNZE KWA MAGAVANA WENZAKE KUTOKA RWANDA, KENYA, BURUNDI (AMBAYO DHAMANI YA FEDHA YAKE NI MARA MBILI YA TANZANIA KWA SASA)
KILIO CHETU KWA WANAUCHUMI NA WATALAAM WA MAMBO YA FEDHA NI MSIACHE KUMPA MAWAZO HUYU GAVANA NAMNA YA KUMANAGE FOREX. HATUSEMI HAJUI LAKINI KILA MTU ANAHITAJI MAWAZO YA KITAALAM. LABDA WA CHINI YAKE WANAMWOGOPA AU ANAWADHARAU. KUNA VIJANA WATAALAM. VYUO VIKUU NA IFM NA WENGINE MPO WAPI AU MNAMWOGOPA? TUMIENI VYOMBO VYA HABARI KUTOA MASOMO KWA WATENDAJI, VIONGOZI, WABUNGE N.K ILI UCHUMI WA NCHI UENDESHWE KISAYANSI NA KISASA.
WATAALAM MSITUACHE! TUTAANGAMIA SIKU ZA KARIBUNI.
KAMA HATUNA FOREX TUTANUNUAJE MBOLEA? TUTAPATAJE CHAKULA KINACHTOKANA NA UAGIZAJI DISELI YA KULIMA? TUTAGIZAJE MITAMBO, TUTATIBIWAJE HUKO INDIA N.K TUTAAGIZAJE MADAWA?
tUTAENDELEAJI KUOMBA MISAADA AMBAYO KILA MWAKA KIASI KINAPUNGUA KWA KUWA WAKUBWA NAO WANAKABILIWA NA MITIKISIKO YA FEDHA?
WATAALAM WA NJE NA NDANI POPOTE MLIPO MTUSAIDIE SISI WATANZANIA. KILA TATIZO LINA UFUMBUZI WAKE KIAINA.