23 January 2012

Afya ya Asamoah yazidi kuimarika

FRANCEVILLE, Gabon

MSHAMBULIAJI Asamoah Gyan  anaendelea kupona majeraha ya nyama za paja yanayomkabili
, baada ya kufanya ya juzi kufanya mazoezi na kikosi cha Ghana katika fainali za Mataifa ya Afrika.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Marekani (AP), Shirikisho la Soka la nchi hiyo lilisema juzi kuwa Gyan anaendelea vyema baada ya wachezaji wote 23 wa Black Stars kufanya mazoezi mjini Franceville.
Kabla ya taarifa hiyo ushiriki wa Gyan katika mechi ya ufunguzi ya Ghana, dhidi ya Botswana katika mechi za Kundi D ulikuwa kwenye hatihati baada ya kuumia mwanzoni mwa mwezi huu.
Hata hivyo Ghana inasisitiza kuwa mshambuliaji huyo, anaendelea vyema baada ya kupatiwa matibabu wakati timu hiyo ikiwa kambini Afrika Kusini chini ya mataalamu kutoka Serbia, Marijana Kovacevic.

No comments:

Post a Comment