13 December 2011

Waislamu kuandamana nchi nzima

*Wapinga maridhiano ya serikali, makanisa
*Wataka Mahakama ya Kadhi


Na Rehema Maigala

UMOJA wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu nchini, umeandaa maandamano nchi nzima kwa madai ya kupinga mkataba uliofikiwa  kati ya Serikali na makanisa ili
kutoa huduma za kijamii, elimu na afya.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kiongozi wa umoja huo Bw.Kondo Bungo, alisema mkataba huo umelenga kuifilisi nchi na kutajirisha makanisa husika.

Alisema maandamano hayo yamepangwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu ambapo mkataba huo, hauna ridhaa ya wananchi ndio maana Serikali imeufanya siri kwa kuyapa makanisa mabilioni ya fedha ili kuimarisha huduma hizo.

“Lengo jingine la kufanya maandamano haya ni kushinikiza uwepo wa Mahakama ya Kadhi ambayo itawezeshwa na Serikali kama ilivyo katika nchi nyingine.

“Huduma katika hospitali nyingi za Serikali zimedorora sasa badala ya kuziimarisha, wao wanatoa fedha nyingi na kuzipeleka kwenye makanisa ili yajiimarishe katika shule na hospitali zao,” alisema.

Aliongeza kuwa, Tanzania ni nchi maskini tangu ipate uhuru ambapo bajeti ya Serikali zaidi ya asilimia 60 inatokana na fedha za wahisani na nyingine wanakopa katika taasisi za fedha.

Bw.Bungo alisema, huduma za afya na elimu ambazo zinatolewa na makanisa ni miradi yao ndio maana hakuna hospitali wala shule za kanisa zinazotoa huduma bure ambapo mapato ya miradi husika yanatumika kuimarisha makanisa hayo.

Alisema maandamano hayo kwa wakazi wa mikoani, yataelekea katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa husika ambapo Dar es Salaam yataanzia Mnazi Mmoja kwenda katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Mizengo Pinda.

“Zaidi ya miaka 20, madai haya yameshindwa kupatiwa ufumbuzi wa kudumu mbali ya kuyafikisha katika ngazi zote muhimu, njia za kidiplomasia zimetumika lakini hazijaleta tija zaidi ya kudharauliwa, kukebehiwa na kupuuzwa hivyo tumeona ni vyema tuwakilishe madai yetu kwa kufanya maandamano,” alisema.

24 comments:

  1. Mh! I doubt if there is any truth in the so called contract or based on rumors!

    ReplyDelete
  2. it may be rumors, however, the truth is that so many regardless of their faith have benefited from these so called "mashule na hospitali za makanisa", thus, govt providing subsidies to these hospitals and schools is not immoral at all, since they are assisting govt to provide social and health services. Acheni mawazo potofu, hospitali za miskiti nazo hazija nyimwa ruzuku, tatizo you have not invested much in those areas that's why you tend to be against the scheme.

    ReplyDelete
  3. Tatizo ni kwamba sisi ambao siyo wa makanisa hatufanyi bidii ya kujiendeleza tunabaki kupiga mayowe tu bila vitendo. Tubadilike na sisi tuache uvivu wa kufikiria.

    ReplyDelete
  4. nafikir watazania lazima tuwe waangarifu tusije tukachanganya ukabira na dini katika utanzania wetu katika miaka hii hamsini ya uhuru. lamsingi tuungane tuungane tusonge mbele tiuimarishe uchumi wetu.

    ReplyDelete
  5. Kweli jamani serikali inalaumiwa bure, kumbukeni ilitoa majengo ya TANESCO Bure Morogoro Kwa ajili ya Kuanzisha Chuo Kikuu. Je hao wa makanisa wamepewa wapi Bure Zaidi ya Harambee na Michango ya Waumini wao.Jamani Igeni Harambee hizi ili tujenge na kuboresha huduma kwa jamii

    ReplyDelete
  6. Wanaofanya maandamano inabidi wawe makini wasije kuwaumiza waumini wao wenyewe. Mathalani, mkoani Tanga ambako waumini wengi ni wa dini ya Kiislam bado hao hao wameomba kuwepo kwa hospitali teule zinazomilikiwa na makanisa. Mfano mzuri ni Wilaya ya Kilindi ambao walikuwa na uchaguzi wa kujengewa hospitali ya serikali. Lakini wananchi wale wakiongozwa na mashehe wao walimuomba askofu wa Lutherani (ambaye wakati huo hakuwa hata na kanisa huko Kilindi) wajengewe hospitali ya kanisa ili iwe hospitali teule ya Wilaya hiyo. Maeneo ya Wilaya hiyo wamezoea kwa miaka mingi huduma zinazotolewa na makanisa. Wanajua tofauti ya ubora wa huduma za hospitali za serikali kama ilivyo Handeni na zile za kanisa (japo ndogo) za Kwediboma na wilaya ya Kilosa kule Berega. Haya andamaneni, lakini atakayepata hasara hasa atakuwa muumini wa kawaida kabisa wa Kiislamu ambaye kwake yeye huduma ya afya na uhai wake ni bora zaidi kuliko kujua nani hasa anaitoa. Bila ruzuku ya serikali hospitali hizi zitaendelea kuwepo lakini raia wengi, wakiwemo waislam watashindwa gharama zake. Hayo yatakuwa ni moja ya matokeo ya kufanikiwa kwa maandamano haya. Mimi nayaombea maandamano yafanikiwe kabisa ili ukweli ujulikane. Penye ukweli uwongo utajitenga.

    ReplyDelete
  7. Hao wana lao jambo wameona mchakato wa katiba unakaribia wamehamasishwa na waraaabu waandamane ili wadai mahakama ya kadhi. Huduma za hospitali ni danganya toto tu, warudishe Chuo kikuu cha majengo ya tanesco kabla ya kuilalamikia serikali juu ya huduma za jamii zinazotolewa na makanisa. Warudishe kwanza hiyo university waliyopewa na serikali bila kuigharamikia ndipo tutaanza hadith za maandamano ya mahakama ya kadhi. Hawa ni watu wa shari. Ni shari za waarabu hizo. Angalia wamemua Gadafi wakidai wanalipa kisasi wakati alikuwa anawasaidia sana. Wasituletee watanzania shari za uarabuni. Waandamane watakutana na mkono wa dola. JK amewaelimisha weee wapi. Tatizo la watu wasiokwenda shule. Madrasa hayawezi kuwasaidia bila elimu dunia. Kwani uwezo wenu wa kufikiri utaendelea kuwa mdogo tu siku zote badala yake mtatumia jaziba.

    ReplyDelete
  8. Maandamano hayo ni mwendelezo wa fikra finyu na potofu zenye kujenga chuki katika jamii yetu. Huduma za makanisa, shule na hospitali mnazozilalamikia zimejengwa katika misingi ya kuhudumia wananchi wote bila kujali dini ama kabila. Hata wanaowashawishi kuandamana wanaujua ukweli huo. Fikirieni namna ya kuanzisha huduma kama hizo na mzitoe pasipo ubaguzi wa dini muone kama hazitakubalika na kuendelea. Tatizo mnatanguliza udini ambao kamwe hauwezi kukuza taasisi za kijamii, mfano halisi ni hicho chuo kikuu cha kupewa bure, kinazidi kudorora na kudidimia siku hadi siku. Tanzania haina ubaguzi wa dini, tuendeleze huduma za afya bora, elimu, n.k. pasipo kubaguana. Hakuna hata madaktari wanaofundishwa kutibu watu kwa misingi ya dini zao. Sasa sijui mtaandamana kudai serikali ifungue vyuo vya kufundisha madaktari, mahakimu, waalimu, n.k. wa kuhudumia kwa misingi ya dini. Kesho tutasikia maandamano kupinga barabara zinazoelekea kwenye makanisa. Maandamano kupinga mabomba ya maji kuelekea sehemu fulani, ili mradi tu kuonyesha wanaonewa wakati jamii ya kitanzania imechanganyika vema. Malalamiko hayajengi bali fikra sahihi na utambuzi wa mazingira halisi na kuchapa kazi kwa tija. Mungu ibariki Tanzania, Amani hii ni lulu isiyopaswa kuchezewa. Asiyejua thamani ya amani hii aulize hata kwa wanaotoka nchi jirani.

    ReplyDelete
  9. Nadhani hayo maandamano yana ajenda ya siri. Nilidhani wanataka kuandamana kupinga mkataba ambao sidhani upo anyway. Sasa si nao wajenge shule na hospitali waone kama serikali itakataa kuwapa ruzuku, waachane na madrasa na misikiti mikubwa isiyo na tija pekee yake. Pia nashangaa kuwa wanaongelea kupinga shule na hospitali za makanisa lakini hapohapo wanaingiza ajenda ya kadhi. Sasa haya maswala mawili yanaendana vipi? Kwa hiyo hii yote ni kuvuruga tu sherehe ya wakristo ya krismasi. Hawana lolote na hawana agenda.

    ReplyDelete
  10. Namuomba M/mungu anijaalie nifike hiyo siku ya Tarehe 23 Disemba ili na mimi niungane kwenye hayo Maandamano na Inshallah yasisite mpaka tupate tunachodai iwe kama Syria au Misri Inshallah...

    ReplyDelete
  11. Ama kweli fikra finyu haijifichi. Watu wazima wanashindwa kuchanganua mambo eti kisa in udini. Serikali inawekeza mahali ambapo wananchi wote wanapata huduma bila kujali dini rangi au jinsia. Sasa mahakama ya kadi ni kwaajili ya waisilamu tuu hivyo sio busara kwa serikali kuwekeza huko maana kodi ni zetu sote. Leo serikali ikiwekeza kwenye hizo mahakama za kadhi basi kutakuwa hamna shida wala lawama serikali ikianza kujenga makanisa ambayo yatanufaisha jamii moja tuu. Watanzania wenzangu embu amkeni na kuangalia mambo kwa mapana yake tusije wote tukatumbukia shimoni kwa kutojua kuchanganua mambo. Wala hauitajiki weledi wa hali ya juu kufahamu mambo ya msingi kama haya.

    ReplyDelete
  12. Hivi UMOJA wa Wahadhiri wa Dini ya Kiislamu upo chini ya BAKWATA? maana mi nashangaa kila siku wanaibuka watu wapya, mara kamati ya kutetea mali za waislama mara nini? hivi hamna utaratibu? hamna chombo kinachowaunganisha?

    mi nafikiri mngeendamana kutaka mafisadi washtakiwe na kutaka katiba mpya, kweli nyie hamnazo, endeleeni kujenga misikiti na madrasa, sie tunasonga, chuo kikuu cha morogoro kinazidi kudorora nafikiri hata TCU wanweza kukifuta hakina Hadhi kabisa
    sasa serikali ikitoa ruzuku kwa makanisa ndio mpewe hiyo ruzuku kwa mahakama ya kadhi?

    ReplyDelete
  13. mwandishi umekosea, sema waislam wasio na upeo wa kufikiri kuandama nchi nzima, mimi ni musilam siwezi kuandamana kwa ujinga huo. Mahakama ya Kadhi ikiianzishwa inanisaidia nini mimi? itanipa kula au kazi au itaniondolea umaskini wangu? napoenda KCMC kutibiwa sijawahi kuulizwa dini ndiyo nitibiwe, mwanangu mwenyewe kasomea udaktari pale na hawakumkataa kwa sababu muislam.
    Ndugu zangu baada ya maandamano mfanye na harambee ya kukichangia chuo chetu cha morogoro

    ReplyDelete
  14. Tazama roho butu zinavyowaongoza watu na hata fikira zao kuwa butu.
    hiki kinachoitwa mkataba kimsingi ni makubaliano ya ushirikiano (memorandum of understanding)katika utoaji huduma za kijamii na hasa Afya kati ya serikali na makanisa. hili lilifanyika baada ya serikali kuona kwamba si rahisi kufikisha huduma hizi kila mahala kwa mara moja na kwa kuwa mashirika mengi ya dini yana hospitali na vituo vya afya maeneo ya vijijini na pembezoni mwa nchi basi nibora kukubaliana na kuona serikali isaidieje ili kuboresha utoaji wa huduma hizi kwa wote.wanaotibiwa huko si wakristo tu hata dini ya mtu haiulizwi lakini pia ghalama za uchangiaji si kubwa hivyo, kimsingi ni msaada kwa raia wetu. Jamani tumuogope mungu kuchanganisha hata kwa mambo mazuri yanayofanyika.hata leo hao wanaosema waandamane ninuhakika wakienda maeneo ya waislam kuliko na huduma hizi za makanisa waislam wenzao watawafukuza maana hawawatakii heri kwa hayo wanayoyahubili.kwa mimi ninavyofikiri swala la mahakama ya kadhi lisilinganishwe na haya mambo ya huduma za afya.
    mahakama ya kadhi ni sehemu ya ibada ya kiislam na haiwezi kutumiwa na mtu mwingine asiye muislam . kama ni hivyo kwa nini waislam wasijivunie kuanzisha kitu hiki na wakighalimikie.kwa welevu wangu mkuu wa mahakama zote zilizopo na zilizoanzishwa kwa utaratibu wa kawaida ni jaji mkuu. sasa fikirieni kama mtataka ianzishwe na serikali manayake sikumoja akitokea jaji mkuu mkristo basi aitawale pia mahakama yenu nafikili acheni kufikiri vya dezo kaeni imarisheni bakwata na ifanyeni mahakama ya kadhi kuwa muhimili wa bakwata ila mdai maamuzi yake yatambulike katika mfumo wa sheria

    ReplyDelete
  15. Hapa ndo patamu ,Jk andaa askari wa kutosha km unavyopiga wanachadema wanapoandamana vivyohivyo upambane na hawa wauni, wanadai makanisa yanapendelewa embu jiulize je kuna hospital yoyote ya islam yenye hadhi ya kuwa hospitali teule au deferral .kumbe kanisa linasaidia serikali kutoa huduma ya jamii.mbona chuo cha Morogoro wanafunzi wanaosoma pale nao wanapata udhamini wa serikali?nawashauri wajenge vyou vingi na maospiotal haswa kwenye wilaya ambazo hazina hospitali za wilaya waone km hawatapata rusuku

    ReplyDelete
  16. jamani kuna jumuiya za kiislamu zinafanya vizuri, lakini kabla hatujaandamana tuandamane kuleta mapinduzi bakwata kwanza, matatizo ya waisilamu yanaletwa na bakwata, viongozi hawana uwezo, wapo kwa ajili ya matumbo yao, wameuza mali nyingi sana za waisilamu, laiti tukipata uongozi bora bakwata hapatakuwa na shida tulizo nazo, mbona wenzetu wameweza, mchawi ni bakwata tu

    ReplyDelete
  17. Maandamano yao hayana hoja. Wamesahau mwembechai. Huduma zinazotolewa haziangalii dini ya mtu. Tatizo la waislamu ni shule. Wanakariri tu!Wafanye kazi kwa bidii wasome elimu dunia. Nchi hii haitakuwa milele nchi ya kiislamu wale ya kikristo. Tanzania itabaki nchi ya dini zote.

    ReplyDelete
  18. Upuuzi tu. Hizi District Designated Hospitals (DDH) pamoja na nyingine zinazomilikiwa na mashirika ya kidini (mainly christian)zimeokoa maisha ya waTanzania wengi sana.. waumini wa dini mbalimbali na wasioamini. Hakuna dhehebu au dini waliozuiwa kuanzisha utoaji wa huduma za afya. Pale ambapo serikali iliona kuwa haina resources za kutosha kujenga hospitali, lakini kuna hospitali ya shirika la dini, kitu ilichofanya ni kuingia mkataba na mashirika hayo ya dini ili kutoa huduma za afya kwa wananchi wa sehemu hiyo. Mifano ni mingi saana..KCMC, Bugando, Peramiho, Ndolage, Mvumi, Nyangana, Mugumu, Lushoto nk nk.

    Ndugu zangu Waislamu, jengeni hospitali kama KCMC, Bugando nk. Nina hakika serikali itasaidia kama mlivyopewa Chuo cha TANESCO Morogoro buuure!

    ReplyDelete
  19. waislamu kuweni kama mbaiwayu ukipewa ushauli unachanganya na zako si kila ushauli ni mzuli hizo huduma za kijamii huwa zinatumika na wote tena nyie wenyewe mashaidi sasa mtaka kugoma nini mtaka wakristu nao wajenge madrasa za biblia sio hivyo bwana tuwaunge mkono walete maendeleo mfano chuo cha st.agustino,tumain,st.joseph.teku pamoja na hospitali nyingi za wakritu lakini na waislamu wengi wanapata huduma hapo usigome changanya na akili zako.

    ReplyDelete
  20. ni jambo lililowazi kuwa katika nchi hii waislam na uislamu unapigwa vita kwa siri na dhahiri,waisalmu kunyimwa haki ya kuanzisha vyuo au mahospitali, mahakama ya kadhi ambayo kwao ni WAJUBU kama sehemu ya ibada na ndio maana wanaidai kwa nguvu,lakini pia kuna ubaguzi ndani ya nchi hii kuwagua waislamu kwa kuwanyima fursa mbalimbali. huu ni muendelezo wa mabaki ya wakoloni na baba wa taifa ambaye yeye ndio aloondoa mahakama ya kadhi iliopo kabla uhuru na kuanzisha bakwata,baada ya kuvuruga mipango ya waislamu kuanzisha chuo chao kikuu kabla ya kile cha udsm chini ya east african muslim walfare society (EAMWS).
    lakini mbali na hayo tutambue kuwa, waislamu wanafuata dini yao kwa mujibu wa muongozo kutoka mtume wao na wala sio watu wakuvamia mambo kama watu wengine, hayo ni maagizo ya dini yao.
    ni vuzuri ufahamu kwa kina jambo unaloliongelea kabla ya kuzungumza, bila ya kufahamu uislamu huwezi kujua nini waislamu wanadai.utaendelea kushabikia mambo tu. lakini hapa ni kudhihirisha upinzani wazi wazi. inashangaza kuwakejeli waislamu kuwa hawana elimu kwa sababu madrasa na misikiti ndo imewalaza akilii, sasa wanaojidai wameelimika tumekuta kule loliondo kwa babu wameach mahospitali waliojenga.

    ReplyDelete
  21. mbona hata waislamu nao walijaa loliondo na wengi wamepona huku walidai hiyo ni shilka fanya utafiti kabla ya kulaumu

    ReplyDelete
  22. inshallah MNYezi Mungu akusaidie wewe mwenye akili finyu kama panya ambaye unaunga mkono maandamano kupinga maendeleo ya nchi hii. kwani naamini bila hospitali na shule za makanisa tusingalikuwa na akina JK na wewe mwenyewe ungekuwa marehemu kwa surua na polio.Muulize Jk alipata wapi hiyo elimu iliyo muweka hapo japokuwa uwezo wake kutekeleza mambo ni mdogo.

    ReplyDelete
  23. Nyinyi vichwa maji ambao mnawalaumu waislam kwamba hawakuwa na mipango, ndio maana hawana huduma za jamii someni vizuri historia ya nchi hii, hayo mabilioni waislam ndio walikuwa wa kwanza kuyahitaji wakati wa utawala wa Baba yenu wa taifa lakini walikataliwa.Tunataka kodi zetu wote zitunufaishe.jk ana uwezo mkubwa mnoo,huwezi kumfananisha na wale waliotufanya hadi tukakosa sabuni, nguo,sukari eti kuvipata hadi upange foreni? kwa hakika hawa watu walikuwa na uwezo mdogo kweli

    ReplyDelete
  24. Jamani, hakuna faida yoyote katika udini, wivu, na blablaa zisizo na msingi wala ukweli wowote, tuungane katika nia moja kulijenga Taifa letu! Bora kuandamana kwa ufisadi kuliko kuandamana kupinga maendeleo!

    ReplyDelete