Na Mwajuma Juma, Zanzibar
UONGOZI wa timu ya Miembeni SC, umeondokewa na wachezaji tisa kutokana na usajili wao kutokamilika.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Msemaji wa timu hiyo Sadi Justin, alikiri kuondoka kwa wachezaji hao ambao alisema sita ni kutoka Tanzania Bara na watatu wa Zanzibar.
Sadi alisema kuondoka kwa wachezaji hao ni pengo kubwa kwa timu hiyo ambayo inakabiliwa na michuano ya Ligi Kuu.
“Hakuna sababu nyingine iliyowaondoa wachezaji hawa, ila tatizo hili linatuumiza vichwa," alisema.
Alisema kutokea tatizo hilo, uongozi wa timu utaitisha kikao kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi.
“Tutakaa kulijadili suala hili kwa ajili ya kuwarudisha wachezaji hawa na baadaye tutajipanga kwa ajili ya usajili wa dirisha dogo," alisema Justin.
No comments:
Post a Comment